Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Familia ya Uncle Zumo wote waigizaji

UKIPENDA muite Mohammed Kingara ‘Uncle Zumo’. Huyu ni mmoja wa wachekeshaji hapa Bongo aliyejizolea mashabiki wengi, ndani ya miaka minne tangu aanze kuigiza amaeonyesha kuwa na mafanikio katika tasnia hiyo.
Hii ni pamoja na kubebea tuzo katika kipengele cha chaguo la watazamaji iliyotolewa kwenye tuzo za filamu mwaka huu jijini Mbeya.
Mwanaspoti imefanya naye mahojiano, amezungumza mambo mbalimbali ikiwemo safari yake ya sanaa huku kubwa kutaka kujua ilikuwaje familia yake yote kujiingia kwenye uigizaji.
Zumo aliingia kwenye sanaa mwaka 2017, kwa kuchekesha kupitia mtandao wa Instagram akiwa ameshawishiwa na mmoja wa rafiki zake.
Anasema wakati wanaigiza na rafiki yake huyo, mtoto wake anayejulikana kwa jina la Mai Zumo naye akawa analilia kuigiza na walipokuwa wakimruhusu kufanya hivyo kwa nia ya kumbembeleza ili asilie, waliona anapatia na hapo ndipo waliamua kumuingiza kwenye uigizaji.
Wakati mama yake Habiba ambaye tayari alishawahi kuwa muigizaji akianzia shule, naye akaungana naye na kujikuta sasa familia nzima inaigiza.


Wanatengaje muda wao
Licha ya kuwa waigizaji, Zumo anasema kila  mtu ana shughuli zake anafanya.
Hivyo katika ratiba zao, anasema huwa wanafanya mazoezi Jumamosi na kurekodi Jumapili, wakati kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa, kila mtu anakuwa kwenye shughuli zake zingine za kutafuta riziki huku Mai naye akipata muda wa kwenda shule na wanaporejea nyumbani usiku kila mmoja akitoa mawazo yake ya nini cha kufanya wiki ijayo.


Mitandao ya kijamii
Kama alivyosema kuwa umaarufu wake aliupata kupitia mitandao kwa kurusha vichekesho, anaeleza kumemsaidia kwa kiasi kikubwa sio tu kufahamika bali kufanya kazi na watu wengine.
“Ni kujulikana kupitia mitandao ya kijamii, hivi sasa ninaonekana katika tamthiliya ya Jua Kali huku Mai akiwa anaonekana kwenye tamthilia ya Kapuni.
“Pia familia yangu kwa nyakati tofauti tunapata madili ya matangazo mbalimbali hivyo kwetu mitandao ya kijamii sio sehemu tu ya kuburusisha watu bali ni ofisi," anasema.
Uncle Zumo anasema walau uigizaji wa sasa umebadilika kutoka miaka minne waliyoanza kazi hiyo.
“Katika uigizaji wa sasa, wengi wanaigiza mambo yenye uhalisia tofauti na miaka ya nyuma, ila changamoto ni kwamba licha ya wasanii kujitahidi kuboresha kazi zao, kinachowakwamisha ni soko ikiwemo kazi zao kununuliwa kwa bei chee.
“Mfano mnunuaji ananunua filamu moja kwa Sh 1 milioni, utalipa nini wasanii, bodi ya filamu na tozo na kodi nyingine zinazohitajika ndio hapo watu wanakimbilia kwenye tamthiliya lakini nazo zikiwa nyingi, watu watakuwa wanalipua ilimradi wapate hela,” anasema msanii huyo.


Kushinda tuzo
Anagusia siri ya kuwa mshindi katika tuzo za filamu ni kutokana na kuwapa kile wanachopenda watazamaji na kusisitiza kuwaomba wampigie kura huku akiwaahidi kutowaangusha kwani walimwamini kumpa ushindi huo.


Kuhusu Comedy Bongo
Anasema bado watu hawajaipokea kihivyo tasnia ya uchekeshaji, kwani ni kama wasanii wanachekesha tu halafu watu waendelee na shughuli zao, wakati wanaume kuigiza kama wanawake anasema sio mbaya lakini sio msanii ajiweke kwa jinsi hiyo sana hadi kuwakera watazamaji.


Mbali ya kuigiza
Ni fundi wa kutengeneza magari, ni dereva ambaye aliwahi kuendesha gari zinazokwenda Kusini mwaka 2010 hadi 2011 na pia aliwahi kuendesha daladala huku akisema msanii anayemvutia duniani ni Mr Bean na Tanzania ni Marehemu King Majuto.


Historia
Zumo alizaliwa mwaka 1985 jijini Dar es Salaam huku elimu ya msingi akiipata Kilwa Masoko, kabla ya kujiunga na shule ya Sekondari Kibiti iliyopo wilayani Rufiji, Pwani.
Hata hivyo akiwa kidato cha pili hakufanya vizuri katika mitihani yake jambo lililomlazimu kwenda kujifunza ufundi gereji.