Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Elton John kutumbuiza hata baada ya kifo chake

ELTON Pict

Muktasari:

  • Inadaiwa Elton John atarekodi maonyesho maalumu mwaka huu katika studio za Pinewood kabla ya taswira yake kubadilishwa kuwa hologram yenye mwonekano halisi.

LAS VEGAS, MAREKANI: MWANAMUZIKI nguli wa Uingereza, Elton John anatarajiwa kuendelea kuwaburudisha mashabiki wake hata baada ya kifo chake baada ya kuripotiwa kusaini mkataba wa mamilioni ya Pauni wa matumizi ya teknolojia ya hologram.

Kwa mujibu wa taarifa mbalimbali, maonyesho hayo yatafanyika katika Hoteli mpya ya Hard Rock mjini Las Vegas, Marekani, itakayofunguliwa mwakani. Teknolojia itakayotumika inaelezwa kuwa ya kisasa zaidi kuliko ile iliyotumika katika maonyesho ya ABBA Voyage yaliyofanyika London.

Inadaiwa Elton John atarekodi maonyesho maalumu mwaka huu katika studio za Pinewood kabla ya taswira yake kubadilishwa kuwa hologram yenye mwonekano halisi.

ELT 01

Wasanii kama Dua Lipa na Kiki Dee, waliowahi kushirikiana naye katika nyimbo maarufu, pia wanatarajiwa kuwa sehemu ya maonyesho hayo.

Chanzo kimoja kilieleza kuwa mradi huo utakuwa tofauti na maonyesho ya kawaida, ukilenga kuwapa mashabiki uzoefu mpya wa burudani kwa kutumia teknolojia ya hali ya juu.

Hatua hiyo imewashangaza wengi kutokana na kauli aliyowahi kuitoa Elton mwaka 2018 aliposema hataki kuona hologram yake ikifanya maonyesho duniani baada ya kifo chake. Wakati huo amesema alimwomba mtoto wake mkubwa, Zachary, kuhakikisha jambo hilo halitokei.

ELT 02

Elton John alistaafu rasmi ziara za muziki mwaka 2023 baada ya kumaliza ziara yake ya Farewell Yellow Brick Road. Hata hivyo, bado amekuwa akifanya maonyesho machache, licha ya kukiri hivi karibuni kuwa uwezo wake wa kuona umeathiriwa na maambukizi ya jicho.

Iwapo mpango huo utakamilika, Elton John atakuwa miongoni mwa wasanii wakubwa duniani ambao wataendelea kutumbuiza kupitia teknolojia ya hologram hata baada ya kufariki dunia.