DStv yazindua Zigo la sikukuu kwa mashabi wa soka na filamu

Dar es Salaam.  Mashabiki wa soka nchini watabahatika kuona mechi Zaidi ya 100 za ligi kubwa duniani kupitia kampeni ya Zigo la sikukuu iliyozinduliwa na kampuni ya Multichoice Tanzania.

Promosheni ya Zigo la sikukuu inamwezesha Mtanzania kuunganishwa kwa Shs. 59,000 na zawadi ya kifurushi  kipya cha DStv Poa  kwa muda wa mwezi mmoja bila malipo.

Kupitia promosheni hiyo, mashabiki wa soka watapata fursa ya kuona mechi moja kwa moja za Ligi kuu ya Uingereza (EPL), Laliga, Italia (Serie A), Ligi ya nabingwa Ulaya na Europa.

Mkuu wa msoko wa MultiChoice Tanzania, Roland Shelukindo alisema kuwa  ofa hiyo imekwisha anza na itamalizika mwishoni mwa mwezi Januari, mwakani.

“Tunafahamu kuwa kipindi hiki cha sikukuu watu wengi usafiri kuungana na familia zao maeneo mbalimbali mijini na vijijini na kwa kulitambua hili tumejipanga kuhakikisha huduma zetu zinapatikana kirahisi kila mahali,” alisema Shelukindo.

Alisema kuwa promosheni hiyo pia ina lengo la kuwawezesha Watanzania wengi wanapata huduma hiyo ili waweze kufurahia burudani elimu na habari wao na familia zao msimu huu wa sikukuu.

“Kila unapofika msimu wa sikukuu hutoa ofa maalum kwa wateja wake ili kuwapa uhakika wa kupata huduma za DStv kipindi hiki ambapo ni cha sikukuu na watu wengi wakiwemo watoto huwa likizo hivyo kuwepo kwa uhitaji mkubwa wa burudani nyumbani.

Alisema kuwa mbali ya mpira, pia watanzania wapata fursa ya kuona  ya kupata burudani mbalimbali kuanzia filamu, tamthilia mpya  za kinyumbani kama Danga na La Familia, bila kusahau filamu za kimataifa.

“Pia kutakuwa na vipindi bora vya watoto ambao sasa wanaanza likizo ikiwemo cartoon network, Disney, Nickelodeon, CBeebies, Boomerang, JimJam na Davinci zikiwa kwa Lugha ya kingereza wakati chaneli  ya Mambo Moto sasa inakuletea vipindi bora vya Watoto vilivyotafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili.