Diamond ashinda tuzo ya Msanii Bora Afrika

Summary

  • Mwimbaji wa Bongofleva toka WCB Wasafi, Diamond Platnumz amefanikiwa kushinda tuzo ya Msanii Bora wa Mwaka Afrika (African Artiste of The Year) kutoka Ghana Music Awards UK usiku wa kuamkia leo.

Mwimbaji wa Bongofleva toka WCB Wasafi, Diamond Platnumz amefanikiwa kushinda tuzo ya Msanii Bora wa Mwaka Afrika (African Artiste of The Year) kutoka Ghana Music Awards UK usiku wa kuamkia leo.

Diamond alikuwa anawania kipengele hicho na wakali wengine Afrika kama Burna Boy, Davido, Wizkid, Master KG, Fireboy, Patoranking, Sinach, Mercy Chinwo, Judikay na Teni.

Hata hivyo, Diamond hakuweza kuhudhuria hafla ya utoaji wa tuzo hizo kutokana na kuanza ziara yake ya muziki nchini Marekani hapo juzi ambapo atafanya shoo 11 hadi Oktoba 31, 2021.

Ushindi huo unakuja baada ya hivi karibuni kutajwa kuwania tuzo za All Africa Music Awards (AFRIMA) na African Muzik Magazine Awards (AFRIMMA), kote anawania vipengele zaidi ya vitatu.

Ikumbukwe mwaka huu Diamond alikuwa ndiye msanii pekee Tanzania na Afrika Mashariki kuchaguliwa kuwania tuzo za BET 2021 katika kipengele cha Best International Act na ushindi kwenda kwa Burna Boy wa Nigeria.

Imeandikwa na Peter Akaro.