Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Diamond aingia tuzo za Grammy

DIAMOND Pict

Muktasari:

  • Wimbo huo umeachiwa Agosti 30, 2025 na hadi sasa video yake imetazamwa zaidi ya mara milioni nne ikiwa nafasi ya 15 kwenye video za muziki zinazotazamwa zaidi duniani kwa sasa.

MWANAMUZIKI kutoka Marekani, Ciara amewasilisha kazi mbili kwenye tuzo za Grammy zinazotarajiwa kufanyika mwaka 2026, kati ya hizo moja ni ngoma ya Low aliyomshirikisha nyota wa Tanzania, Diamond Platnumz.

Wimbo huo umeachiwa Agosti 30, 2025 na hadi sasa video yake imetazamwa zaidi ya mara milioni nne ikiwa nafasi ya 15 kwenye video za muziki zinazotazamwa zaidi duniani kwa sasa.

Ngoma hiyo iko kwenye albamu ya 'Cici' yenye nyimbo 18, huku Low ikiwa ni moja ya inazofanya vizuri ambayo ni kolabo pekee kufanya na msanii kutoka Afrika.

Wimbo huo umewasilishwa katika vipengele viwili ambavyo ni Best Music Video pamoja na Best African Music Video hivyo kuna uwezekano ngoma hiyo ikapitishwa kwenye kipengele mojawapo.

Pia albamu yake ya Cici imewasilishwa katika kipengele cha Best Progressive R&B Album, villevile wimbo wake Ecstasy aliyomshirikisha Normani na Teyana Taylor, umeingia katika kinyang’anyiro cha vipengele viwili vya muziki wa R&B ambavyo ni Best R&B Song na Best R&B Performance.

Tangu aanze kuimba muziki mwaka 2000, Ciara amechukua tuzo ya Grammy mara moja mwaka 2006 ambapo alishinda kupitia wimbo wa 'Lose Control' aliowashirikisha Missy Elliott na Fatman Scoop ulioshinda kipengele cha Best Short Form Music Video.