Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Davido na mkewe wapata mapacha

Staa wa mziki, David Adeleke maarufu kam Davido na mpenzi wake Chioma, wamejaliwa kupata watoto pacha ikiwa ni miezi kadhaa imepita tangu wafiwe na mtoto wao wa kwanza.

Davido alionekana mwenye furaha akiwa na Chioma alipokwenda kumpokea hospitali.

Licha ya kutotajwa jinsi zao, lakini mmoja anaonekana ni wa kiume na mwingine wa kike kwa namna walivyovalishwa kofia zao.

Mastaa hao wanapata watoto hao ikiwa imepita miezi kumi tangu wafiwe na mtoto wao wa kwanza wa kiume aliyejulikana kwa jina la Ifeanyi (3), aliyepata ajali ya kudumbukia kwenye bwawa la kuogolea.

Tangu wakati huo, Chioma hajawahi kuonekana kuwa na ujamzito mpaka jana usiku picha na video zao kusambaa katika mitandao mbalimbali zikiwaonyesha kutoka hospitali wakiwa na watoto wao pacha.