Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Cudi: Diddy alipojua natoka na Cassie, gari langu likachomwa moto

DIDY Pict

Muktasari:

  • Kid Cudi amesema gari lake la kifahari aina ya Porsche liliunguzwa moto na nyumba yake kuvunjwa baada ya Sean Combs kugundua kuwa alikuwa akitoka kimapenzi na Cassie Ventura.

NEW YORK, MAREKANI: Msanii wa muziki Kid Cudi, mtaalamu wa vipodozi mashuhuri, na mfanyakazi wa hoteli walikuwa miongoni mwa waliotoa ushahidi Alhamisi kuhitimisha wiki ya pili ya kesi ya uhalifu wa kimtandao na usafirishaji wa binadamu kingono inayomkabili Sean “Diddy” Combs katika mahakama ya shirikisho.

Rapa huyo, anayejulikana mahakamani kama Scott Mescudi, alitoa ushahidi uliotikisa zaidi siku hiyo. Alimshutumu Combs kwa kuivamia nyumba yake na kuhusika katika kuteketezwa kwa gari lake la kifahari aina ya Porsche, ambalo liliunguzwa kwa kupigwa bomu la Molotov nje ya nyumba yake.

Waendesha mashtaka walitumia mashahidi hao kuimarisha madai ya msingi yaliyotolewa na Cassie Ventura, mpenzi wa zamani wa Combs, ambaye alitoa ushahidi wiki iliyopita.

Hadi sasa, waendesha mashtaka wameita mashahidi 16 katika kipindi cha wiki mbili. Kesi inatarajiwa kuendelea Jumanne baada ya mapumziko ya wikiendi ya Memorial Day Marekani kwa ushahidi kutoka kwa Capricorn Clark (mkurugenzi wa zamani wa masoko wa Combs) pamoja na maafisa wa polisi wa LAPD na LAFD.

Waendesha mashtaka wamedai kuwa Combs na baadhi ya watu wa karibu naye walitumia vitisho, vurugu, dawa za kulevya, hongo, uchomaji moto, utekaji nyara na uongo kuwashinikiza Cassie Ventura na mwanamke mwingine kushiriki katika sherehe za kingono alizozita “Freak Offs” na kulinda sifa ya tajiri huyo wa muziki.

Upande wa utetezi umekiri kuwa Combs alikuwa mkatili kimapenzi kwa wapenzi wake, na wakati wa taarifa ya ufunguzi walisema alikuwa na “maisha tofauti ya kingono.” Pia walikiri kwamba, ingawa Combs ni “mtu mwenye upungufu mwingi,” hakufanya uhalifu wa shirikisho unaodaiwa.

Ushahidi wa Alhamisi:
Kid Cudi alipoingia mahakamani akiwa amevaa jaketi la ngozi, hakuonekana kuangaliana macho kwa macho na Combs alipopita kuelekea kizimbani. Combs alibaki akiangalia mbele.

Mescudi (41) alisema alikutana na Ventura mwaka 2008 na walikuwa wapenzi kwa muda mfupi mwaka 2011. Alishuhudia kuwa aliamini kuwa wakati walianza kuchumbiana, Ventura hakuwa tena katika uhusiano wa kimapenzi na Combs. Ventura alimweleza kuwa Combs alimshambulia kimwili.

Desemba 2011, Ventura alimpigia simu “akiwa na hofu” saa 12 asubuhi akisema Combs alikuwa amegundua uhusiano wao. Kwa hofu kwamba Combs angemfuata Mescudi, walihamia katika hoteli ya jirani.

Ventura alisema wiki iliyopita kwamba alikuwa kwenye “Freak Off” (mapenzi ya kikundi) na Combs alipopata habari za uhusiano wake na Mescudi. Alisema Combs alikasirika sana, alijaribu kumshambulia kwa kifaa cha kufungua mvinyo, lakini alifanikiwa kutoroka na Mescudi alimchukua.

Wakiwa hotelini, waligundua Combs na mtu wake wa karibu walikuwa ndani ya nyumba ya Mescudi.

Mescudi alimkabili Combs kwa simu: “Wewe m******, uko nyumbani kwangu?”
Combs alijibu: “Nataka tu kuzungumza na wewe, niko hapa nakusubiri.”

Cudi akadai waliporudi nyumbani, Combs hakuwepo, lakini alikuta kamera za usalama zilikuwa zimehamishwa, zawadi zilikuwa zimefunguliwa, na mbwa wake alikuwa amefungiwa chooni. Aliita polisi na kutoa taarifa ya uvamizi.

Baada ya Krismasi, Cudi anasema walitengana Cassie Ventura kufikia Mwaka Mpya.

Januari 2012, Mescudi alipigiwa simu na mlezi wa mbwa wake akamwambia Porsche yake ilikuwa inawaka moto. Mahakama iliangalia picha za gari lililoharibika vibaya.

“Ilionekana kama juu ya paa la Porsche palikuwa pamekatwa na bomu likapitishwa hapo,” Mescudi alisema.

Mkutano wa faragha ulipangwa kati ya Mescudi na Combs katika Soho House, LA.
Alipoulizwa kwanini aliomba mkutano, Mescudi alisema, “Nilijua alihusika.” Upande wa utetezi ulipinga, na hakimu alikubaliana na pingamizi hilo.

Combs alikataa kuhusika na alisema, “Sijui unachozungumzia,” alipoulizwa kuhusu gari. Mescudi alisema alihisi Combs alikuwa anadanganya.

Mwaka 2015, walikutana tena, na Combs aliomba msamaha.

UHUSIANO NA CASSIE VENTURA
Mescudi alisema alikuwa akizungumza na Ventura karibu kila siku kwa mwaka mzima. Walipoachana Desemba 2011, “tulikatisha mawasiliano.”

Akiulizwa na wakili wa utetezi kama “alitapeliwa kimapenzi,” Mescudi alikubali kwa neno moja: “Ndiyo.”

Katika maswali ya ufuatiliaji, Mescudi alisema waliachana kwa sababu ya drama zilizovuka mipaka. Alisema alikuwa na hofu kwa ajili ya usalama wake na wa Ventura “kwa sababu nilijua Sean Combs alikuwa mkatili.”

USHAHIDI MWINGINE
Zemmour (Meneja wa Hoteli ya L’Ermitage), alisema walihifadhi taarifa za tabia mbaya za Combs:
“Humimina nta kila mahali na hutumia mafuta mengi.”
“Alichafua sana chumba wakalazimika kufanya usafi wa kina kila alipoondoka.”
“Aliidhinisha $1000 ya ziada kwa uharibifu wa chumba alioufanya.”

MTAALAMU WA VIPODOZI
Mylah Morales, mtaalamu wa vipodozi kwa watu mashuhuri, alitoa ushahidi Alhamisi kuhusu tukio la mwaka 2010 kati ya Sean Combs na Cassie Ventura, ambapo Combs alidaiwa kuwa na tabia ya ukatili baada ya kuhudhuria sherehe nyumbani kwa msanii Prince.

Tukio hilo lilielezwa kwa mara ya kwanza na Ventura alipotoa ushahidi tarehe 14 Mei. Alisema alienda kwenye sherehe nyumbani kwa Prince bila kumwambia Combs. Baadaye, Combs alivamia chumba cha hoteli alikokuwa Cassie, akampiga na kumrushia mizigo.

Akiwa kizimbani Alhamisi, Morales alisema Combs aliingia kwenye chumba cha hoteli walichokuwa wakikaa na kuuliza, “Yuko wapi huyo k**a?” Kisha aliingia chumba kimoja na Ventura na kufunga mlango. Baada ya muda mfupi, Morales alisikia kelele za kupiga mayowe na kilio.

“Nilipatwa na mshtuko, na sikujua la kufanya,” alisema.

Baadaye, Combs alitoka chumbani kwa hasira na Ventura alikuwa “amesononeka sana” na alikuwa amejeruhiwa, alisema Morales.

MSAIDIZI WA ZAMANI WA DIDDY
George Kaplan, aliyekuwa msaidizi wa mtendaji wa Combs, ambaye alianza kutoa ushahidi wake Jumatano na akaendelea Alhamisi, alisema aliacha kazi hiyo baada ya kushuhudia ukatili wa Combs dhidi ya Ventura na mwanamke mwingine.

“Sababu kuu ya kuacha kazi kama msaidizi wa Bw. Combs ni kwamba sikuwa na amani wala kukubaliana na tabia za kimwili (za ukatili) ambazo niliziona mara kwa mara kwa miezi kadhaa,” alisema Kaplan.

Alisema hakutaka kushiriki katika “kuficha au kusuluhisha aina hiyo ya mambo.”

Kaplan, aliyekuwa akitoa ushahidi chini ya agizo la kinga ya kisheria (immunity), alisema alifanya kazi katika kampuni ya Combs Enterprises kuanzia mwaka 2013 hadi Desemba 2015.

Alieleza kuwa alishuhudia Combs akimshambulia Ventura mwishoni mwa mwaka 2015 kwenye ndege binafsi. Katika tukio jingine, Combs alimuita Kaplan bafuni, ambako alimkuta Ventura analia kitandani, akiwa ameshika kichwa chake huku akiwa na alama za kupigwa usoni. Alikiri kuwa hakuchukua hatua yoyote wala kuita polisi.

Aidha, mwishoni mwa mwaka 2015, Kaplan alisema alimuona Combs akiwa amekasirika akirusha ma-apple kwa mpenzi mwingine aitwaye Gina. Hakuweza kusema kama ma-apple hayo yalikuwa ni matunda halisi au ya mapambo.

Licha ya matukio hayo, Kaplan alisema bado huwasiliana na Combs na humtumia salamu kila mwaka siku ya bethidei yake. Alisema kazi hiyo ilikuwa “nafasi ya kipekee maishani” na aliongeza kuwa alikuwa “na shukrani kubwa kwa mafunzo” aliyoyapata kutoka kwa Combs.

Wakati wa ushahidi wake, Kaplan alikuwa akimtazama Combs mara kwa mara, na wawili hao walionekana kutabasamu kwa kila mmoja. Alipokuwa akitoka mahakamani, Kaplan alimkazia macho Diddy na kumsalimia kwa kumuinulia kichwa, naye Diddy aliijibu kwa kumuinulia kichwa pia.