Ben Pol atoa kibao cha kimahaba

Saturday July 17 2021
ben pic

MSANII wa bongo Fleva, Ben Pol ametoa kibao kipya kinachokwenda kwa jina la Warira, kikizungumzia mahusiano ya watu walioachana na mmojawapo anakumbuka mema ya mwenzake.
Ben Pol amesema wakati anaandika mashairi ya wimbo huo, alikuwa anafanya utafiti wa watu wenye mapenzi ya dhati na inapotokea wakatengana, kunakuwepo na nyakati za kukumbukana.
Amesema anaamini ujumbe wake utawagusa wengi ambao wanapitia nyakati za kutengana angali wanapendana na kujua makosa madogo madogo hayana budi kutokea, lakini wanastahili kuvumiliana.

ben pic 1


"Ninapotunga nyimbo kama hizi hazina maana kwamba zinahusiana na mimi moja kwa moja badala yake namaanisha kwamba ni maisha ambayo ni kawaida katika jamii zetu ndio maana nafanya kazi ambayo itaelimisha na kuburudisha pia, "Ndani ya nyimbo hiyo, inazungumzia wapenzi wawili mmoja alikuwa msumbufu kisha wakatengena na huyo msumbufu  anaanza kujuta na kuomba msamaha wa kubadilika" amesema Ben Pol.
 


Advertisement