Baraka the Prince: Muziki ni maisha, naimba maisha

Thursday June 23 2022
prince pic
By Olipa Assa

MSANII wa Bongo Fleva, Baraka the Prince amesema anatumia uwezo wake wa kuimba na kuandika, kuufanya muziki kuwa maisha kwa mashabiki wanaopenda kazi zake.

Amesisitiza muziki ni maisha, hivyo kabla ya kuandika nyimbo zake anafikiria ujumbe utakaokwenda kuishi kwa jamii anayoipelekea kazi zake.  

"Sifanyi kazi kwa kushindana na mtu mwingine, ninachokizingatia ni ujumbe ninaoupeleka kwa jamii inayousikiliza na kuutazama muziki wangu," amesema Baraka the Prince na kuongeza;

"Muziki ni maisha ndio maana kila binadamu ana chaguo lake na msanii anayemtaka iwe nyimbo za kijamii ama za dini, jambo la msingi ni kuelewa wanapenda kusikia kitu gani kutoka kwangu,"

Baadhi ya  nyimbo zake zilizowahi kutamba sana ni Siwezi, Siachani Nawe, Jichunge, Mazima, Namkumbuka na nyingine nyingi.

Advertisement