Baba Levo amuomba Mambosasa kuharakisha uchunguzi wa kesi yao na Harmonize

Muktasari:

Msanii Clayton Chipando maarufu kwa jina la Baba Levo, amemuomba Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa kuharakisha upelelezi wa kesi waliofunguliwa na msanii Harmonize.

Msanii Clayton Chipando maarufu kwa jina la Baba Levo, amemuomba Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa kuharakisha upelelezi wa kesi waliofunguliwa na msanii Harmonize.

Baba Lebo ameyasema hayo jana Jumamos Mei1, 2021 alipozungumza na waandishi wa habari.

Ikumbukwe Aprili 16,202, Baba Levo pamoja na wenzake wakina Rayvanny, Juma Lokole waliitwa na kuhojiwa kituo cha Polisi Central kutokana na kulalamikiwa na Harmonize kuhusika kusambaza mitandaoni picha za utupu zinazodaiwa kuwa ni zake.

Zikiwa zimepita siku 15 tangu walipohojiwa Baba Levo anamuomba Mambosasa kuharakisha upelelezi na kumpeleka Mahakamani kwa kile alichosema asingependa jambo hilo likaishia polisi.

"Nimemtajaa moja kwa moja Kamanda Mambosasa katika uharakishaji wa kukamilisha upelelezi kwa kuwa yeye ndio aliujulisha umma kupitia vyombo vya habari kuwa wametuhoji na uchunguzi bado unaendelea.

"Hivyo ningependa tukutane mahakamani,kwani nimechoka kuripoti Polisi kila wakati na pia ananichelewesha kupata fidia yangu ya Sh6 bilioni nitakayomdai Harmonize kwa kunidhalilisha kwa jambo ambalo sijahusika nalo," amesema Baba Levo.

Mbali ya kuhojiwa na Polisi katika sakata hilo la Harmonize, pia msanii huyo alijikuta akitozwa faini ya Sh1 milion kutokana na kuimba wimbo ulioonyesha kumlenga Harmonize japo sababu iliyotajwa na Baraza la Sanaa la Taifa(Basata) ni kwamba haukuhaririwa na wao kabla haujaachiwa hewani.