Alikiba kutumbuiza Fainali Mapinduzi Cup

Wednesday January 12 2022
kiba pic
By Mwanahiba Richard

UNGUJA. Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Alikiba kesho Alhamisi anatarajiwa kutumbuiza kwenye fainali za Kombe la Mapinduzi zitakazoanza saa 2:15 usiku Uwanja wa Amaan kisiwani hapa.

Fainali hiyo inazikutanisha Azam FC na Simba baada ya kushinda michezo yao ya nusu fainali ambapo Azam iliitoa Yanga kwa penalti 9-8 wakati Simba iliifunga Namungo FC bao 2-0.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindani hayo Imane Osmond Duwe kuwa mbali na Alikiba pia kutakuwa na burudani mbalimbali kutoka vikundi vya sanaa kisiwani hapa.

"Kutakuwa na burudani mbalimbali kwenye fainali hizo hizo lakini kubwa ni Alikiba msanii mkubwa kutoka Bara. Ni fainali za aina yake msimu huu na yamekuwa na ushindani mkubwa tangu yalipoanza," amesema Imane

Advertisement