Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Alicia Keys awapoza mashabiki wa Diamond

Muktasari:

Toleo la kwanza la wimbo wa Wasted Energy lilitoka mwezi Septemba likiwa ni moja ya nyimbo zinazopatikana kwenye albamu ya Alicia Keys. Ambapo humo ndani Diamond aliimba kipande kidogo cha sekunde 10 tu katika wimbo wa dakika 4 na sekunde 19.

HATIMAYE povu la mashabiki wa Diamond dhidi ya mwanamuziki wa Marekani, Alicia Keys la kumuimbisha kidogo msanii wao kwenye wimbo wake aliomshirikisha mwezi Septemba limetoa matunda baada ya msanii huyo kuachia remix ya ngoma hiyo, safari hii Diamond ameimba muda mrefu.

Mabadiliko yaliyofanyika kwenye wimbo huo ulitoka leo Ijumaa Desemba 18, 2020 si tu ya Diamond kuimba vya kutosha, bali pia ameongezwa msanii mwingine kutoka Marekani anayefahamika kwa jina Kaash Paige, kwahiyo jumla remix hiyo ina wasanii watatu.

Dakika chache baada ya kuachia wimbo, Alicia Keys alituma video inayomuonyesha akiwa studio akisikiliza wimbo huo na kuambatanisha maneno; "Mliomba wimbo huu! Hakika mapenzi yenu juu ya Wasted Energy ni ya moto sana. Na sasa Diamond na Kaasha Paige wamefanya mambo makubwa humu ndani,


Kuhusu ngoma ya kwanza
Toleo la kwanza la ngoma hiyo lilitoka Septemba likiwa ni moja ya nyimbo zinazopatikana kwenye albamu ya Alicia Keys, ambapo humo ndani Diamond aliimba kipande kidogo cha sekunde 10 tu katika wimbo wa dakika 4 na sekunde 19.

Jambo hilo lilipelekea mashabiki wa Diamond kuvamia kurasa za mitandao ya kijamii ya Alicia na kulalamika kwa kilichofanyika.

Hata hivyo, mapovu yalipozidi, mume wa Alicia Keys, prodyuza Swizz Beatz alimuomba Diamond awatulize mashabiki wake kwa kuwaeleza ukweli kuwa ni yeye mwenyewe Diamond ndiye aliyechagua kuimba kipande kidogo.

Kupitia mtandao wa Instagram huko huko, Diamond aliweka wazi kwamba kuna kazi nyingine nyingi kati yake na staa huyo zinakuja.

Aidha, mpaka sasa takwimu zinazoonyesha wimbo wa Wasted Energy unapendwa zaidi ya wimbo wowote kutoka kwenye albamu hiyo ya Alicia Keys kwani ndiyo wimbo uliotazamwa zaidi.