Afande Sele atekeleza agizo la Rais Samia

Muktasari:

  • Taasisi hiyo itahamasisha pia upandaji wa miti ya matunda ili jamii ifaidike zaidi na sio kupanda miti kwa matumizi ya kivuli na mazao na wanaamini watashirikiana vyema na taasisi nyingine za serikali na binafsi kukabiliana vita ya  mabadiliko ya tabianchi hapa nchini na dunia kiujumla.

AGIZO la Rais wa Tanzania, Dk Samia Suluhu Hassan la kumtaka mfalme wa rhymes katika muziki wa kizazi kipya nchini kutunga nyimbo zenye kuhamasisha utunzaji wa mazingira zimeanza kutekelezwa baada ya mfalme huyo kutunga wimbo maalumu wa kutunza mazingira.

Akizungumza katika uzinduzi wa ofisi na  wimbo maalumu leo Julai 6, 2023 mkoani Morogoro, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Afande Sele Foundation (ASEFO), Seleman Msindi amesema uzinduzi wa ofisi hizo ni hatua ya utekelezaji wa viongozi wa juu kumtaka kutunga nyimbo zenye kuzungumzia utunzaji wa mazingira.

Afande Sele ambaye ni Mfalme wa Rhymes muziki wa kizazi kipya amesema, Rais Dk Samia pamoja na Makamu wa Rais wa Tanzania, Dk Philip Mpango kwa nyakati tofauti wamemtaka mfalme huyo kutumga nyimbo za kutunza mazingira ili jamii iwe inapata elimu ya utunzaji mazingira kupitia kipaji chake

“Leo tumezindua rasmi wimbo maalumu wa mazingira pamoja kuzindua ofisi za taasisi ya Afande Sele Foundation (ASEFO) hapa Chamwino Manispaa ya Morogoro na lengo letu ni kuleta mageuzi katika utunzaji wa mazingira tukishanda miti tutahakikisha miti inalelewa kama anavyolelewa mtoto kwa kuhakikisha makuzi ya miti hiyo inajitegemea baada ya kupata huduma nzuri ili isife.”amesema Afande Sele.

Mkurugenzi wa Unganisha Enironment Conservation Organization (UECO), Sophia Kalinga amesema ujio wa taasisi hiyo itasaidia kuongeza nguvu katika kutoa elimu ya utunzaji wa mazingira nchini.

“Adhari za uharibifu wa mazingira ni tatizo kubwa kwa jamii ambayo haina elimu ya kutosha ya utunzaji wa mazingira licha ya juhudi za kutoa elimu ya utunzaji wa mazingira inatoa mwanga baada ya serikali, taasisi binafsi na mashirika kusimama kidede kutoa elimu ya kutunza mazingira nchini.”amesema Sophia.

Pia Mkurugenzi Mtandaji wa Mtendaji w Chuo cha St Joseph, amesema kuzinduliwa kwa ofisi ya Taasisi ya Afande Sele Foundation ni hatua nzuri ambayo itakuja kuleta mabadiliko ndani ya Manispaa ya Morogoro na Tanzania kiujumla.

“Moja ya mambo mnayopaswa kuyafanya uongozi wa taasisi hii ya ASEFO ni kuwa taasisi ya mfano kwa kuanza kupanda miti na kuitunza ili kupata msitu utaokuwa wa mfano kwa mashirika, taasisi binafsi na serikali za utunzaji wa mazingira kuiga kama njia ya kukabiliana na maeneo yaliyoharibiwa.”amesema Chomoka.

Chomoka ambaye ni mgeni rasmi katika uzinduzi huo amesema jamii inahitaji zaidi kujifunza kwa vitendo na pale watapoona mfano halisi ni tasisi kuiga na kuleta manufaa ya pamoja kwa wao kupanda miti na kuitunza.