Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

‘Uno la Chibu linamkondesha Zari’ yateka wimbo mpya wa Harmonize

Muktasari:

Harmonize ametoa wimbo wake mpya unaitwa Uno huku mashabiki wake wakivutiwa na mstali ulipomtaja boss wake wa zamani Diamond na Zari.

Dar es Salaam. Mwanamuziki Bongo Fleva, Harmonize anayemiliki lebo ya Konde Gang ametoa audio ya wimbo wake unaoitwa 'Uno'.

Katika wimbo huo Harmonize amewataja wasanii mbalimbli akiwemo aliyewahi kuwa boss wake Diamond Platnumz, aliyewahi kuwa mpenzi wa Diamond Zari, mbali na hao pia mwanamuziki Ray C, Gwajima, na mwanamuziki wa nchi ya Kongo Fally Ipupa.

Harmonize ametoa wimbo huo leo katika akaunti yake ya Youtube na kupata comment nyingi za mashabiki zake.

Comment nyingi zinazosomeka ni pale alipomtaja Diamond na Zari kitu ambacho watu baadhi kushangwa na wengine kudai hawa wasanii ni watu ambao wapo kibiashara.

Baadhi ya Comment za watu walioandika ni hizi: Issa Mwero"Kama umeskia uno LA #chibu_ linamkondesha #zari ebu gonga like apo chini twende sawa na uno"

Ramadhani Lianje "Uno la chibu linamkondeshaga zari# km unaamini hawa watu hawana bifu gonga like tukamatie uno"

Jonathan Mj ameandika "Gonga like apa kama umesikia eti Uno la chibu linamkondesha Zari"

Salum Nanyenje"Kwel kondeboy hana ugomvi na chibu (simba)"

Geofrey Elph Jr "Kama umeskia CHIBUUU gonga like twende sawa????"