VIBE LA WIKI : Tukio la Gomes na matibabu yetu ya barafu!

Muktasari:
Son alionekana mpaka kubembelezwa na wachezaji wengine na hata madaktari waliongia uwanjaini lakini hakutana kuelewa na alionekana kujuta kufanya jambo lile, lakini kwa hapa kwetu kuna baadhi ya wachezaji wanapenda kucheza rafu mara kwa mara bila kujali afya za wenzao.
INAAMINIKA soka ndio mchezo unaopendwa na watu wengi duniani kwani hata katika viwanja vya michezo huo mashabiki hufurika na hata katika maeneo mengi si jambo la kushangaza kuona kuna vikundi vya watu wakibishana kuhusu mchezo.
Katika kuhakikisha mchezo wa soka ndio unapendwa zaidi kwa mfano hapa Tanzania unaweza kuwakuta watu katika vijiwe mbalimbali, ofisini na mahala pengine wakibishana na kutaniana kuhusu mchezo wa soka haswa katika timu mbili za Simba na Yanga na muda mwingine ligi pendwa na England ambapo kuna timu za Chelsea, Man City, Liverpool, Arsenal, Manchester United na nyinginezo.
Mchezo huo wa soka umeweza kutengeneza mastaa wengi katika dunia ambao wamekuwa vipenzi vya watu katika jamii husika mpaka huamua kuingia katika siasa kama aliyekuwa kipa wa TP Mazembe Moses Kidiaba ambaye kwa sasa ni Mbunge nchi DR Congo.
Mchezo huo wa soka ni miongoni mwa mchezo ambao unaongoza kulipa wachezaji mkwanja mwingi huenda na ukawa miongoni mwa michezo mitatu ya juu ambayo inalipa pesa nyingi wachezaji, makocha na wengine wanaohusika.
Soka mbali ya kupendwa na watu wengi umekuwa miongoni mwa mchezo hatari ambao mara chache unaweza kutokea jambo baya ambalo kila mmoja anaweza kushangaa na kuingiwa simanzi kama vifo ambavyo viliwakuta mchezaji kinda wa Mbao, Ismail Mrisho Khalfan na mchezaji wa timu ya Taifa ya Cameroon Marc Vivien Foe.
Ukiachana na matukio hayo ya vifo ambayo yalikuwa simanzi na kusisimua dunia nzima, wiki hii ilitokea tukio lingine la kusisimua katika mechi ya ligi ya England kati ya Everton na Tottenham Hotspur ambapo kiungo wa Andre Gomes alivunjika mguu. Tukio hilo la kuvunjia vibaya mguu kwa kiungo wa Everton Gomes si mara ya kwanza kutokea katika mchezo pendwa wa soka kwani liliwahi kuwakuta wachezaji wengine kama Djibril Cisse, Luke Shaw, Seamus Coleman na wengine wengi.
Katika tukio hilo Wino mweusi limeona kuna mambo ya kujifunza haswa kwa wachezaji, madaktari, mwamuzi na mashabiki waliokuwa karibu na tukio hilo la kuvunjika kwa Gomes. Jambo la kwanza la kujifunza kwa wachezaji ni ile hali ya udhuni na kujuta kwa tukio la kucheza rafu ambalo alikuwa akionesha mshambuliaji wa Tottenham Hotspur Mkorea Son Heung-min, ambaye mpaka alionekana kumwaga machozi na kujuta tukio la kumchezea rafu Gomes.
Son alionekana mpaka kubembelezwa na wachezaji wengine na hata madaktari waliongia uwanjaini lakini hakutana kuelewa na alionekana kujuta kufanya jambo lile, lakini kwa hapa kwetu kuna baadhi ya wachezaji wanapenda kucheza rafu mara kwa mara bila kujali afya za wenzao.
Katika ligi za ndani hapa nchini si jambo la kushangaza kumuona mchezaji akimchezea rafu mwenzake tena mbaya huku ikiwa kwa makusudi na hata baada ya tukio hilo anachukulia kuwa ni jambo la kawaida kwa tukio la kuvunjika kwa Gomes na hali aliyooneshaa Son wachezaji wa kwetu wanatakiwa kujifunza.
La kujifunza lingine beki wa kulia wa Tottenham Hotspur, Serge Aurieria nae alifanya jambo la haraka kuita madaktari baada ya kumuona Gomes amepata majeraha hayo mabaya maana alikuwa karibu nae alifanya jambo la haraka kuwaita madaktari huku akionekana akitumia nguvu ili wafike haraka na kutoa guduma ya kwanza. Jambo lingine la kujifunza mshambuliaji wa Everton, Cenk Tosun baada ya kuona mguu wa Gomes amevunjika alikuja kwa haraka mno katika eneo la tukio na kumshika kichwa cha Gomes kwa mambo mawili kwanza kumuangalia asiumize ulimi lakini kumtaka asiangalie jiraha lake ambalo alilipata.
Jambo hilo la Tosun kumshika kichwa Gomes huku akiwa anaongea nae hunda alifanikiwa kumfanya asimize ulime wake jambo ambalo lingesababisha madhara zaidi hata kupoteza maisha lakini kupunguza maumivu kwa wakati ule kama angekuwa anajiangalia katika jeraha lake ambalo lilikuwa ni kubwa.
Wachezaji wa kwetu wanatakiwa kuangalia tena zaidi ya mara moja na kujifunza kwa Tosun, ambaye kwangu alifanya jambo sahihi kabisa na hata wachezaji wa kwetu Tanzania wanatakiwa kuelewa hilo na siku ikitokea tukio kama hilo waweze kulifanya na si kuanza kumuangalia mchezaji aliyepata tatizo la aina hiyo.
Tukio lingine kubwa lilikuwa ni huduma ambayo walikuja kutoa madaktari waliofika kumpatia huduma ya kwanza Gomes, walikuwa zaidi ya saba na walikuja na vifaa sahihi ambavyo kila mmoja alikwenda kuhusika na jambo lake sahihi.
Madaktari walimpatia huduma ya kwanza na kumtoa uwanjani Gomes akiwa amebebwa katika machela, huku akiwa anasikiliza maumivi yake mbalimbali na hata mashabiki wote bila kujali utofauti wa timu zao na walimpigia makofi. Hapa kwetu Tanzania inaweza kutokea kuna mchezaji amemua utamuona daktari au madaktari wanaingia uwanjani kumpatia huduma ya kwanza wakiwa na maji au barafu mkononi na hata muda mwingine zile dawa ambazo wanakuwa nazo si sahihi.