MKEKA WAKO : Halina ubishi Manchester City itaipiga Man United

Muktasari:

Manchester City ndio wanakamata nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu England wakati Manchester wanashika nafasi ya sita.

Timu mbili zenye upinzani wa jadi za Manchester City na Manchester United zinavaana kesho Jumamosi kwenye Uwanja wa Etihad kwenye mechi ya Ligi Kuu England.

Pamoja na ukweli kuwa timu hizi mbili zitakuwa zinasaka ushindi ili kuweza kumtambia mwenzake lakini zitakuwa zinasaka nafasi ya kujiweka vizuri.

Kumbuka kuwa upinzani wa kati ya timu hizi ulianza hizo mwaka 1881, ambapo Manchester United iliibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya City.

Manchester City ndio wanakamata nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu England wakati Manchester wanashika nafasi ya sita.

Mabingwa watetezi, Manchester City wana pointi 36 wakati Manchester United wamejikusanyia pointi 21.

Kwa watandika mkeka nadhani hili lipo wazi kabisa kuwa Manchester City wataibuka kidedea katika mchezo huu.

Kuwapa Manchester United ushindi kwenye mchezo huu kwa kweli kunahitaji ujasiri wa kiwango cha juu pamoja na ushindi wao wa mabao 2-1 wa mechi ya juzi dhidi ya Tottenham Hotspur.

Mimi kwa upande wangu natoa asilimia 77% kwa Manchester City kupata ushindi kwenye mchezo huu.

Uwezekano wa mechi hii kumalizika sare ni asilimia 19% kutokana mwenendo wa timu zote.

Ila kwa kweli natoa asilimia 10 tu kwa Manchester United 10% kupata ushindi kwenye mchezo.

Ukilinganisha timu hizi kwa kiwango cha juu inaweza kukusaidia kukupa picha ya hali ya timu hizi mbili.

Katika mechi sita za hivi karibuni Manchester City imefanikiwa kushinda mechi tano na kutoa sare moja.

Kwa upande wa Manchester United wameshinda mechi mbili katika mechi sita walizocheza karibuni.

Katika mechi yao ya mwisho, Manchester City ilifanikiwa kupata ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Burnley juzi tena ukiwa ushindi wa ugenini.

Manchester City ingawa wapo vizuri likija suala zima la mechi za nyumbani katika kipindi cha miezi sita iliyopita, imeshinda mechi 10 kati ya 15.

Kwenye idadi ya mechi hizo zinajumuisha tano ilizocheza Manchester City msimu uliopita kwani ilifanikiwa kushinda mechi tano huku moja ikitoa sare na kufungwa mchezo mmoja.

Katika msimu huu wa 2019/20, Manchester City imeshinda mechi tano kati ya saba nyumbani ikiwa sawa na asilimia 71.

Mechi moja ndio imemalizika kwa sare nyumbani wakati pia ikipoteza mchezo mmoja pia.

Kwa msimu huu, Manchester City imeshinda mechi 10 kati ya 15 kwa msimu huu.

Jambo jingine la kuangalia ni kuwa Manchester City inayonolewa na Pep Guardiola imekuwa na sifa kwa mabao yake mengi zaidi katika kupata katika kipindi cha pili.

Kwa upande wa Manchester United wapo hoi likija suala zima la matokeo kwani haini rekodi ya kuvutia sana nyumbani na huku kwa ugenini ikiwa taabani zaidi.

Manchester United imeshinda mechi nne na kupoteza nne katika mechi ilizocheza miezi sita iliyopita. Mechi sita zilimalizika kwa sare.

Timu hiyo imeshinda mechi moja tu ugenini wakati ikipoteza mechi tatu za ugenini na huku ikiwa na sare tatu.

Kwa kuwasaidia zaidi watandika mkeka ni kuna hatihati ya straika wa Manchester City, Sergio Aguero kucheza mchezo huu.

Waamuzi wa mchezo huu wanatazamiwa kuwa Anthony Taylor, atakayesaidiwa na Gary Beswick, na Adam Nunn na huku mwamuzi wa akiba akiwa Mike Dean. wanaifukuza Liverpool huku Man U wanaitafuta top four. Tusubiri tuone.