STRAIKA WA MWANASPOTI : Huko EPL Liverpool ina shughuli pevu msimu huu

Muktasari:

Safu ya ushambuliaji ana mastaa kama Sadio Mane, Mohammed Salah ambao mpaka sasa wemefunga mabao tisa kila mmoja pamoja na Origi ambaye kwa kiasi kikubwa amekisaidia kikosi hicho.

KLABU ya Ligi Kuu England, Liverpool inazidi kung’ara. Ikiwa ndio kwanza raundi ya 17, Ligi Kuu hiyo imetawaliwa na Liverpool, wakiongoza kwa alama 49, wakifuatiwa kwa karibu na Leicester City yenye alama 39.

Mabingwa watetezi, Manchester City mambo sio mazuri sana na wanakamata nafasi ya tatu na alama zao 35, 14 nyuma ya vinara Liverpool.

Huu ni msimu wa Liverpool kunyakua taji hilo na wasipolipata msimu huu, hawatakaa walipate tena.

Msimu uliopita walikuwa wanaongoza jedwali hivi hivi na baadaye taji hilo likawaponyoka na kwenda kwa City.Natumai msimu huu, mambo hayatakuwa mabaya kama msimu uliopita.

Wana alama 49 na mpaka sasa hawajapoteza mchezo hata mmoja na kilichobaki kazi ni kwao. Kocha Jurgen Klopp ana kazi kubwa ya kuhakikisha wanamaliza wakiwa kileleni na hii itawezekana kwa sababu usajili wake wa miaka mitatu iliyopita ndio unaoonyesha kuzaa matunda kwa sasa.

Safu ya ushambuliaji ana mastaa kama Sadio Mane, Mohammed Salah ambao mpaka sasa wemefunga mabao tisa kila mmoja pamoja na Origi ambaye kwa kiasi kikubwa amekisaidia kikosi hicho.

Safu ya kiungo kuna Naby Keita, Andrew Robertson, Trent Alexander-Arnold, Jordan Henderson, Georginio Wijnaldum ambao wanahakikisha ngome yao haipasuki.

Van Dijk naye aneshikilia ngome ya ulinzi huku Allison Becker akiwa mchumani amehakikisha klabu haijafungwa mechi hata moja.

Katika soka ukizingatia usajili tu, basi maisha yako yako yatakuwa bila usumbufu. Klabu mbili kongwe zinasuasua kila kukicha, Manchester United na Arsenal, hazieleweki kabisa. Mara leo kapata matokeo mazuri, kesho zinapokea vichapo. Uunashindwa kuzielewa kabisa.

Angalau meli ya Klopp imetulia baharini. Anapaswa kuiendesha kwa makini kabla haijapinduliwa na mawimbi. Mpaka sasa ana pointi ambazo akiendeleza ushindi ana uhakika wa kushinda taji msimu huu.

Tofauti ya alama kumi na mpinzani aliye karibu Leicester City ni kubwa mno. Kwa hivyo wachezaji wake Klopp wanafaa kujitahidi vilivyo. Huu msimu ni wao.

Ni wazi msimu huu kama watashindwa kubeba taji, basi wasahau kabisa maana wakati wao ndio huu. Ikumbukwe tangu Ligi Kuu ianze kuitwa English Premier League, Liverpool hawajawahi shinda taji lolote lile.

Mataji ambayo wako nayo ni mataji ya mseto ule wa kitambo. Kwa hivyo iwapo watanyakua taji hilo na wana kila sababu ya kunyakua taji hilo, watakuwa wamejiandikishia historia, hasa kwa wale wachezaji wapo sasa hivi klabuni.

Nyota wa zamani wa klabu hiyo, Steve Gerald na wengine walijaribu kushinda taji hilo lakini walishindwa hadi wakastaafu soka.

Kwa hivyo Kuna kila sababu ya wachezaji waliopo sasa hivi kuandikisha historia. Kumbuka msimu uliopita walishinda taji la klabu bingwa barani ulaya. Itakuwa tamu sana, Tena sana iwapo watanyakua taji hilo la EPL msimu huu. Kazi kwao.

Ni mechi 21 wamebakisha kukamilisha msimu. Mzunguko wa kwanza mechi ambazo wamebakisha ni mechi mbili tu. Iwapo watashinda zote mbili, watasimama kwa alama 55. Mzunguko wa pili wakitafuta alama 40 tu, zinatosha kuwahakikishia taji.

Klopp na wachezaji wake pamoja na mashabiki wote wa Liverpool wana kazi kubwa mbele, huku wakiziacha Man United na Arsenal zikiendelea kutafuta njia ya kuifikia top four.

Tungoje, hatuwezi jua baada ya dirisha la usajili la Januari nini kitatokea.

Liverpool wataweza kulinda ushindi wanaoupata kila mara au watateleza.

Man City wataweza kulinda kulinda taji lao lisiende kwa Liver?

Kuna mengi yanakuja mzunguko wa pili na presha itakuwa pia kwenye nafasi za mwisho kama zilizopo mkiani kwa sasa zitaweza kubadili msimamo na kujinasua.

Siku njema.