Zuchu aingia Naija na ‘Nobody’

Friday October 16 2020
zuchuu pic

Wimbo huo ulioanza kuruka hewani leo Oktoba 16 umepewa jina la Nobody, na umeimbwa na Zuchu akimshirikisha Joeboy, msanii kutoka Nigeria ambaye ametamba na ngoma kali kama vile Begining na Baby.

Mashairi katika wimbo huo yanahusu wapenzi wawili, mwanamke na mwanaume wakielezeana jinsi kila mmoja anavyompa raha mwenzake kwenye penzi lao, kiasi kwamba hata wakijaribu kulinganisha, hakuna mtu aliyewahi kuwafanyia kwa namna hiyo na wala hatotokea.

Wimbo umetengenzwa na prodyuza Tony na Laizer wa Wasafi huku video ikiongozwa na direkta Kenny wa Zoom Extra inayomilikiwa na Diamond Platnumz.

Mfahamu Joeboy

Joeboy ni msanii wa Nigeria ambaye amevuma kwa ngoma maarufu za Baby na Beginginng.

Mbali na kuimba, kingine kilichompa umaarufu Joeboy ni staili ya utengenezaji wa video za nyimbo zake kwa mtindo wa vikatuni.

Advertisement

Zuchu anakuwa msanii wa kwanza Tanzania kuachia ngoma kumshirikisha Joeboy.Hata hivyo inadaiwa kuwa tayari wasanii wengi wa Bongo wamesharekodi naye ngoma kwani mwanzoni mwa mwezi huu alikuwa Tanzania akifanya shoo.

Advertisement