Unene wamzingua Aunty Ezekiel kinoma

Tuesday December 5 2017

 

MWIGIZAJI wa kike wa filamu nchini, Aunty Ezekiel amedai hakuna kitu ambacho hakipendi kama kuwa kibonge, akisema anaponenepa kila anapojiangalia hujichukia kwani hukerwa na unene.

“Mimi sipendi kabisa unene ninaponenepa hujiona mbaya kwani unajikuta hadi uso unakuwa wa mviringo hivi, yaani unabadilika kabisa na kuwa tofauti kama awali. Hivyo kulazimika kufanya mazoezi kwa fujo au kutumia dawa,” alisema.

Msanii huyo anaamini pamoja na kuchukiza, mwigizaji akinenepa kuna uwezekano mkubwa wa kupoteza mvuto kwa mashabiki na kama inatokea hapo hali kama hiyo ni wakati ambao watayarishaji wanashindwa kumchukua kumshirikisha katika filamu kwa kule kukosa mvuto, ndiyo maana anachukia kuwa kibonge.