Umri wa Wema Sepetu wazua utata

Monday September 28 2020
wema pic

Wakati leo Septemba 28 ikiwa ni siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa mrembo Wema Sepetu, huenda siku hiyo ikawa mbaya kwake baada ya raia kumshambulia mrembo huyo kurudisha umri wake nyuma.

 

Hii imetokea leo Jumatatu Septemba 28, 2020 baada ya Wema kupitia ukurasa wake wa Instagram, kuweka picha aliyokuwa amevaa gauni jekundu na kujipongeza kwa kufikisha miaka hiyo 30.

 

Katika picha hiyo ilisindikizwa maelezo: “Miaka 30 malaika, niliahidi kusema ukweli kuhusu siku yangu. Septemba 28, 1990 nilitoka tumboni mwa mama yangu Mariam Athuman Sumbe, nina furaha kusheherekea miaka 30 ya maisha yangu, samahani nilidanganya."

 

Advertisement

Maneno hayo ya Wema yalipokewa kitofauti na watu huku baadhi wakionekana kukerwa na tabia hiyo ya wasanii kudanganya umri wao.

 

Mmoja wa waliotoa maoni yao ni Official Lannet ambaye ameandika: “Kipindi namjua Wema Sepetu nilikuwa mdogo na nafikisha miaka 30 mwakani, kazi kwelikweli jamani.

 

"Ila Tanzania tu wenzetu kwenye masuala ya umri wala hawajaligi ila wasanii wetu mnatuangusha jamani."

 

Mwingine ni Rick Ford aliyeandika: "Unataka kusema ulishiriki Miss Tanzania ukiwa na miaka 16, jamani vitu vingine havina hata logic ujue.”

 

Staystar Raphael ameandika: "Mwili kupungua na miaka inapungua au sio, 2006 niko kidato cha tano, leo bado una 30, uache kutudanganya.”

 

Naye Official Mtani ameandika: "Kwani Wema unahesabu miaka kutoka juu kwenda chini au?"

 

Emma Mtapila ameandika: "Happy B.day Wema, Ila ulishiriki umiss na miaka 16 na siku ya umiss tuliambiwa una miaka 18, sasa imekaaje hii?"

 

Ukiachilia mbali maoni ya watu mtandaoni, pia Wema Mwaka 2018 wakati akisheherekea siku yake ya kuzaliwa pale ukumbi wa Mlimani City, mapambo kwenye meza aliyokuwa amekaa mrembo huyo yalionyesha kuwa ana miaka 30.

Advertisement