Ronaldo aamua kuwekeza kwenye nywele

Muktasari:

Tayari CR7 kalipia Euro 1 milioni kwa mradi huo huku akitarajiwa kuongeza Euro25 milioni zaidi katika kipindi cha miaka mitatu au minne ijayo.

FOWADI matata wa Juventus, Cristiano Ronaldo yupo kwenye pilika pilika za kufungua kliniki ya ubandikaji nywele mjini Madrid huku akimteua mchumba wake Georgina Rodrigues kuwa meneja mkuu.

Kliniki hiyo ambayo shughuli kubwa itakuwa ni kuwasaidia wateja wake waliopoteza nywele, kubandikwa upya, itakuwa na mameneja kadhaa huko Rodriguez akiwa meneja mkurungezi.

Cristiano anaamini tajriba ya Rodriguez, aliyekutana naye akiwa anafanya kazi kwenye stoo moja ya mitindo ya fasheni ya designer mbalimbali, itamsaidia kuhakikisha anatoa usimamizi mzuri.

Kliniki hiyo itawaajiri wataalumu 150 wa masuala ya nywele ambao watalipwa mishahara ya kuvutia. Itakuwa na jumla ya vyumba 18 vya upasuaji kila mtaalumu akiwa na chake na kwa siku kila mmoja atatakiwa kumtibu angalau mteja mmoja.

Tayari CR7 kalipia Euro 1 milioni kwa mradi huo huku akitarajiwa kuongeza Euro25 milioni zaidi katika kipindi cha miaka mitatu au minne ijayo.

“Ukiachana na soka, ninapenda sana masuala ya afya, teknolojia na utafiti. Ni sehemu ambazo ningelipenda kuwekeza. Ndio sababu nimeamua kufungua klinki hii ya kitaalumu kabisa katika Mji wa Madrid na niliishi kwa miaka mingi na kupapenda,” CR 7 kanukuliwa.

Kliniki hiyo ni mjengo wa gorofa sita hivyo ishara tosha sio muundo msingi wa mzaha mzaha.