Prodyuza Bonga aachana na Hamornize

Saturday February 22 2020

Prodyuza Bonga aachana na Hamornize,MTAYARISHAJI wa muziki nchini,Bonga , lebo Lykos Empire,

 

By Rhobi Chacha

MTAYARISHAJI wa muziki nchini, Bonga ametangaza rasmi kuachana na msanii  Hamornize ambapo amejiunga na lebo Lykos Empire ambako ataendelea kuwa mtayarishaji na mwimbaji.
Bonga amesema sababu kubwa iliyomuhamisha ni kutafuta maslahi ya kimaisha na kupata uzoefu zaidi kwa kufanya kazi na watu tofauti tofauti.
"Naomba watu waelewe kwamba sijaondoka kwa Hamornize kwa ubaya wala kutofautiana bali ni kwa lengo la kupanua mawazo na kusaka maslahi zaidi," alisema Bonga
Bonga ni mmoja wa washiriki waliotayarisha wimbo wa Uno wa Hamornize na nyimbo nyingine kama Kushoto Kulia

Advertisement