Mulemule atoboa sababu za kuondoka CP Academia

Muktasari:

Mwanamuziki Mulemule ameanzisha bendi yake ya The Bambazi ili kukuza vipaji vya wanamuziki wanaochipukia pamoja na kuwa huru na kazi zake za muziki.

Dar es Salaam. Mwanamuziki mkongwe wa muziki wa dansi, Mulemule FBI amesema ameondoka vizuri bendi ya CP Academia zamani FM Academia na kuanzisha bendi yake inayoitwa The Bambazi.

Mulemule amesema hayo baada ya kusambaa kwa habari kuwa amegombana na Patcho Mwamba Rais wa Bendi ya CP.

Alisema ametoka katika bendi ili kujitegemea kufanya kazi zake na kukuza vipaji vya wanamuziki wengine wanaochipukia.

"Nimeondoka CP Academia sababu ya kutaka kujitegemea kufanya kazi zangu na sio kwamba kwa sababu ya kugombana na Patcho, nimeona kuna vijana  wapo katika makundi ya muziki wa Bongo fleva  wanavipaji vya kuimba muziki wa dansi na Rhumba ambavyo wanashindwa sehemu ya kuvionyesha" alisema Mulemule

Mulemule alisema bendi ya The Bambazi imeshatoa nyimbo mbili ambazo ni Keshaniambia na 'Monbebe' wiki moja ikiwa maana ya Monbebe ni mpenzi wangu.

Mulemule pindi yuko FM Academia amewahi kutunga nyimbo nyingi moja wapo ni wapambe Nuski na Shida, na bendi ya CP Academia wimbo unaitwa Mama Africa.