Harmonize atamani kuimba na AliKiba

Thursday January 16 2020

Harmonize atamani kuimba na AliKiba-Mwanamuziki Harmonize-MwanaspotiBurudani-

 

By Rhobi Chacha

Dar es Salaam.Mwanamuziki Harmonize amesema anatamani kufanya kolabo na AliKiba kwa sababu anapenda kazi yake.

Harmonize aliyasema hayo akiwa Sinza Kijiweni katika studio yake kuwa, yupo tayari kufanya Kolabo na AliKiba baada ya kumaliza kolabo na msanii kutoka Nigeria, Burna Boy.

“Baada ya kumaliza video ya Kolabo na Burna Boy, sasa natamani kufanya kolabo na AliKiba, sababu ni mtu niliyekuwa nikimfuatilia tangu nilipokuwa mdogo, alikuwa moja ya wasanii walionifanya nipende kuimba," alisema Harmonize

Aidha Harmonize alisema kutaka kufanya kolabo na AliKiba sio kwamba kutaka kumkomesha mtu bali ni kutaka kujifunza kwake na kuweka ushirikiano mzuri alioupoteza kwa miaka mingi.

Amesema wapo watu watakaojiuliza siku zote alikuwa wapi kufanya Kolabo na AliKiba hivyo kutakakujibu swali hilo ni kuendeleza mambo ambayo yaliyopita.

"Matamanio haya ya kutakakufanya Kolabo na AliKiba, isiibue mjadala wa watu kuuliza nilikuwa wapi siku zote kufanya naye na ikiwa ni msanii ambaye nilikuwa nasikiliza nyimbo zake, bali watu wasitake kurudisha mafaili ya nyuma kwa kuhoji kile nilichosema, kwa sasa ni amani na ushirikiano ndio silaha yangu."

Advertisement

Advertisement