Diamond: Ndoa ya esma itufungulie milango mabachela tuoe

Thursday July 30 2020

 

By Nasra Abdallah

Msanii wa Diamond Platnumz ameongea maneno mazito wakati wa sherehe ya maulid ya dada yake Esma.

Sherehe hizo zimefanyika leo Alhamisi Julai 30, 2020 nyumbani kwake Madale Jijini Dar es Salaam.

Katika shughuli hiyo iliyoanza saa moja jioni baada ya mume wake Esma, Yahya Msizwa kuingia nyumbani hapo ambapo alipewa nafasi ya kutambulisha familia yake.

Ilipofika zamu ya Diamond na kutakiwa kuongea chochote alisema,"naomba ndoa ya dada yangu iwe milango ya kuwafungulia wasiooa kama mimi waoe na wasioolewa waolewe.

Pia Diamond ametumia nafasi hiyo kumtaka dada yake huyo kwenda kuilinda ndoa yake na kutosikiliza maneno ya watu.

"Mimi sijawahi kuwa kwenye ndoa lakini nasikia zina misukosuko mingi, naomba ukatulie na kuilinda ndoa yako," amesema Diamond.

Advertisement

Sherehe hiyo ilihudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo wasanii kutoka lebo ya Wasafi akiwemo Lavalava na Zuchu.

Advertisement