Davido apimwa corona hana virusi vya Covid-19

Muktasari:

Mwanamuziki wa Nigeria, Davido amefanya vipimo vya corona hana maambukizi ya virusi Covid-19 licha ya mchumba wake kuambukizwa.

Dar es Salaam. Muimbaji wa Afropop wa Nigeria, Davido amefanyiwa vipimo kwa mara pili na kukutwa hana maambukizi ya virusi vya corona.

Mchumba wa Davido, Chioma Avril Rowland hivi amekutwa na virusi vya ugonjwa corona, licha ya kuwa awali hakuwa na maambukizi.

Davido alitumia ukurasa wake wa twitter Jumatano  na kutangaza kuwa alikuwa amepima virusi vya Corona kwa mara ya pili.

"Nilifanya vipimo vya pili vya virusi vya covid19 tena .... kwa mara nyingine mimi ni mzima "aliandika.

Ijumaa iliyopita, Davido alitumia ukurasa wake wa Instagram kutangaza kwamba mchumba wake alipimwa. Aliandika, "Halo kila mtu! Nilirudi hivi karibuni kutoka Amerika baada kuhairisha tour. Mpenzi wangu Chioma pia alirudi kutoka London hivi karibuni na mtoto wetu.

 "Hatukuwa na dalili na bado tunahisi vizuri, lakini kwa sababu ya historia yetu ya hivi karibuni ya kusafiri, tuliamua kuchukua hatua wenyewe na washirika wetu wa karibu ambao tumekutana nao kwa vipimo vya  COVID-19 mnamo Machi 25.

"Kwa bahati mbaya, matokeo ya mchumba wangu alikutwa na maambukizi wakati wengine wote 31 waliopimwa wapo salama ikiwa ni pamoja na mtoto wetu. Bado tunaendelea vizuri kabisa na bado hajaonyesha dalili zozote zile. "