Barnaba ni gofu na tenisi

Muktasari:

  • Barnaba kwa sasa anatamba na wimbo wake mpya wa Nibusu aliomshirikisha msanii wa kike, Yammi na picha  za wimbo huo zilitrendi kwenye mitandao ya kijamii na aina ya uvaaji wao.

NJE na muziki anaoufanya msanii wa Bongofleva, Barnaba amesema anapenda kuufuatilia mchezo wa gofu na tenisi kwa sababu unachezwa na watu wa sekta mbalimbali, hivyo anaona ana kitu cha kujifunza kutoka kwao.

Barnaba kwa sasa anatamba na wimbo wake mpya wa Nibusu aliomshirikisha msanii wa kike, Yammi na picha  za wimbo huo zilitrendi kwenye mitandao ya kijamii na aina ya uvaaji wao.

Wimbo wa Nibusu ni wa kwanza kwa Barnaba kwa mwaka huu, ambapo umemrejesha kwa kishindo sokoni, kama anavyosema mwenyewe

"Umepokewa vizuri na umenipa nguvu ya kufanya kazi nyingi zaidi kwa mwaka huu," amesema.

Kuhusiana na gofu amesema: "Gofu ni mchezo ninaoufuatilia, kwani unachezwa na matajiri, nina ndoto za kuwa tajiri, hivyo lazima nianze kukaa karibu nao ili nijua nitaanzia wapi kutimiza ndoto zangu."

Ameongeza: "Mbali na gofu kuna tennis pia nikiuangalia huwa nafurahia zaidi aina ya uchezaji wake."

Barnaba amewahi kutamba na nyimbo mbalimbali baadhi yake ni Sorry, Nampenda, Yalaniwe Mapenzi, Hunitaki ambao kaimba na Mbosso, Marry Me kamshirikisha Marioo hizo ni baadhi tu ya nyimbo zake.