Kisa Ali Kiba, Diamond Gavana wa Mombasa afichua skendo!

Tuesday March 19 2019

 

GAVANA wa Mombasa, Ali Hassan Joho ‘Sultan’ kawatuliza jazba wasanii wa nyumbani ambao, amekuwa wakilalamika kuhusu mwenendo wake wa kupenda kuwasapoti sana wanamuziki wa kibongo.

Joho alionekana akiwa na ukaribu mkubwa na mastaa wa bongo hasa Alikiba, Ommy Dimpoz na sasa Nandy akijiongeza kwenye hesabu hiyo.

Gavana huyo amehusika pakubwa kuwasaidia kwenye baadhi ya kazi zao, kuwapa shoo na hata pia kuwasaidia kifedha katika njia mbalimbali.

Japo pia ameonekana kuwa na ukaribu na wasanii wa nyumbani, haiwezi kulinganishwa na wenzao wa bongo.

Kitu hicho kimekuwa kikiwakera sana wasanii wa nyumbani ambao wameishi kukesha wakimkashifu kwa kupuuza vipaji vya ndani na kusapoti vya nje.

Sasa Gavana kajibu kwa kusema, sapoti anayowapa akina Ali Kiba ni mipango tu ya kuwafungulia wasanii wa nyumbani hasa wa Mombasa, milango kule Bongo.

“Kitu ambacho watu hawakielewi ni kwamba, huu ni mpango tu kuhakikisha kuwa mwisho wa siku watu wangu wanakubalika kule Bongo na hivyo nao kufaidi,” amedai Gavana Joho.

 

Advertisement