Kipa wa AFC Leopards afunika tuzo ya mwezi Februari

Wednesday March 14 2018

 

By VINCENT OPIYO

Kipa wa AFC Leopards, Jairus Adira juzi alituzwa mchezaji bora wa mwezi katika klabu hiyo kwa utendaji kazi wake mwezi jana.
Adira aliiwezesha Ingwe kutofungwa katika mechi tatu na mbili ni sare tasa dhidi ya Fosa Juniors ya Madagascar katika Kombe la Mashirikisho japo mabingwa hao mara 13 wakaondolewa awamu ya mapema.
Sare nyingine ilitokea kwenye ushindi wa 2-0 na timu yake ya zamani Sony Sugar na juzi amekuwa michumani kwenye ushindi wa 4-3 baina ya Mathare United.

Kwa tuzo hilo, alipokezwa Kshs10 000, “Ni kipa ambaye ameonyesha kwa nini anastahili kushirikishwa katika mechi zote tangu atie kandarasi hapa Januari,
“Mchango wake umeonekana katika mechi zetu za mwezi jana na huu na tunatumai ataendeleza fomu hiyo kadiri msimu unavyozidi kuendelea,” alisema kaimu kocha Dennis Kitambi.