Gaucho ang'aa Simba Queens ikitesa

MSHAMBULIAJI wa timu ya taifa ya wanawake 'Twiga  Stars', Mwanahamisi Omary 'Gaucho' amegeuka kivutio kwa mashabiki wa Simba baada ya kuiongoza timu ya wanawake ya Simba 'Simba Queens' kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Sayari Queens.

Gaucho ni miongoni mwa nyota waliosajiliwa na Simba kwa ajili ya kuitumikia Simba Queens kwenye Ligi Kuu ya wanawake msimu ujao. 

Mshambuliaji huyo ambaye kwa muda mrefu alikuwa anaichezea Mlandizi Queens alionyesha kiwango bora kwenye mechi hiyo kwa kuwasumbua mabeki wa Sayari Queens huku akipiga pasi mbili zilizozaa mabao hayo ya Simba.

Mchezo huo wa Simba Queens dhidi ya Sayari ni miongoni mwa mechi tatu zitakazochezwa kwenye tamasha la Simba Day leo ambapo mingine miwili itahusu timu ya vijana wenye umri chini ya  miaka 20 na ule wa kikosi cha wakubwa dhidi ya Asante Kotoko