Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Watoto wa Mwana FA kufaidi malezi baab’ kubwa

Muktasari:

Mwana FA amesema hajawahi kuishi na baba yake katika maisha yake yote, hivyo ikifika siku ya kuzaliwa huwa anafikiria vitu vingi

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Mwana FA alipiga stori na Mwanaspoti kuhusu maisha yake, mafanikio na changamoto alizokutana nazo hadi hapo alipofikia.

Mwana FA amesema hajawahi kuishi na baba yake katika maisha yake yote, hivyo ikifika siku ya kuzaliwa huwa anafikiria vitu vingi.

“Mimi sijawahi kukaa na baba yangu maisha yangu yote, nimekuwa naruka ruka sana, mara nakaa kwa shangazi yangu, mara nakaa kwa babu yangu, kwa bibi yangu ndiyo kwetu ilikuwa, kwa shangazi yangu mwingine hivyo," alisema.
Mwana FA amesema malezi anayompa mwanaye ni tofauti kidogo tofauti na yeye kwani mtoto wake anamuona kama mshkaji wake.
Anasema anaamini kuwa wazazi wengi wa sasa wamegundua kuwa ni vizuri zaidi wakawa karibu na watoto wao kuliko wakiwaogopa.
“Namna ambayo maisha mimi nimekua, sitaki mwanangu apitie hata robo yake,” anasisitiza. “Kazi nitakayoifanya ni kumpa mafunzo niliyoyapata kutokana na hatua niliyokuwa naipitia bila yeye kuipitia hiyo hatua.”