We Giggy Money weweee

Friday November 10 2017

 

By RHOBI CHACHA

MWANADADA asiyeishiwa vituko anayetamba na ngoma ya ‘Nampa Papa’, Giggy Money amedai kuwa hapa Bongo bwana demu akijua kuimba na kisha akawa na figa bomba, lazima atusue kama ilivyomtokea yeye.

Giggy amedai uimbaji wa muziki kwa wasanii wa kike unachangiwa na vitu vingi vinavyowaopa ujiko, lakini kubwa ni kipaji, mvuto wa sura na figa kitu ambacho

kwake vimemfanya afike alipo.

“Si unaniona nilivyojaaliwa figa matata, sasa na hiki kipaji cha kuimba si lazima watakaa? Nimeingia kwenye game nimedhamiria, mtarajie ngoma baada ya

ngoma,” alitamba Giggy.

Mwanadada huyo ambaye pia ni mtangazaji alisema anashukuru ngoma yake ya Nampa Papa imepokewa vema na mashabiki pengine kuliko hata ‘Tikisa Supu’ na kuahidi hatawaangusha mashabiki wake.