Koletha awashangaa wanaokata tamaa mapema

Muktasari:

Mwigizaji huyo amefunguka hayo kutokana na kuwapo kwa watu wanaokata tamaa na wanaokatisha wenzao tamaa kutokana na wivu, chuki na fitina.

MWIGIZAJI wa filamu Bongo, Coletha Raymond amesema katika maisha, hakuna haja ya kukata tamaa pamoja na kupitia maisha magumu.

Mwigizaji huyo amefunguka hayo kutokana na kuwapo kwa watu wanaokata tamaa na wanaokatisha wenzao tamaa kutokana na wivu, chuki na fitina.

“Kuna msemo usemao tumia muda mwingi kunoa shoka na tumia muda mchache kukata mti, lakini wengi wanatumia muda mwingi kukata mti. Hapa tafsiri yake usikate tamaa kufanikiwa,” alisema Koletha.

Msanii huyo anasema kuna wakati ni raha mtu kubaki pekee yako ili kufanikisha mambo yako kuliko kuwa na makundi ambayo hayana msaada kwako, akiamini watu ambao hufanya mambo makubwa yenye mafanikio, muda wao utumia wakiwa pekee yao na muda mchache kuwa na watu.