Kiben 10 champagawisha Sister Fey

Tuesday August 7 2018

 

By MYOVELA MFWAISA

MWANADADA asiyeishiwa vituko anayetamba kwenye uigizaji na muziki, Faiza Omary ‘Sister Fey’ amedai eti tangu aanze kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi alikuwa hajawahi kummanika mpenzi wake kama alivyofanya sasa kwa Elias Olystar.

Sister Fey amedai mapenzi ya Elias, ambaye kwa mwonekano ni mvulana mdogo maarufu kama ‘Serengeti boy’ yamemkolea mpaka ameshindwa kujizuia kuonyesha hisia zake kwake.

“Kuna baadhi ya watu wananifuatilia kuhusu mpenzi wangu, naomba waniache kwani nimeamua kufurahisha nafsi yangu na wasubiri ndoa itakapofungwa hivi karibuni, ili kuwakata vilimilimi vyao,” alisema mwanadada huyo.

Sister Fey amekuwa gumzo kutokana na kuwa na uhusiano na msanii huyo wa muziki ambaye ni mdogo kiumri, wengi wakiamini ni kutafuta kiki, lakini mwanadada huyo amesisitiza familia zao zipo katika mipango ya kuandaa sherehe za ndoa.