Janjaroo hataki kumtema Uwoya

PENZI la mrembo wa Filamu za Bongo, Irene Uwoya limemtia wazimu nyota wa Bongo Fleva, Dogo Janja ‘Janjaroo’ ambaye sasa anautumia mfungo huu wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani kuombea ndoa yao idumu.

Janjaroo alisema linapokuja suala la maombi, aliweka wazi kuwa kama mwanadamu haishiwi na mapungufu ambayo ameyatubu kwa Mungu lakini sala yake kuu ni ndoa yake na Uwoya idumu.

“Kama binadamu siishiwi na makosa, lakini katika mfungo huu wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani yapo mengi ambayo nilifanya toba maalum. Kubwa sana ni uhai wa ndoa yangu na Sheila (Irene Uwoya), maana siko tayari kuona ikivunjika,” alisema nyota huyo anayemudu kuimba Hip Hop na RNB.

“Ndoa hii inaniletea furaha katika maisha yangu, kwa hiyo naiweka ndoa yangu kwa Mungu na yote namuachia yeye,” alisema Dogo Janja aliyelelewa na kukuzwa na kundi la Tip Top Connections.

October mwaka jana Dogo janja alifunga ndoa na Irene Uwoya ambaye alimbadirisha dini kuwa Muislamu na kuitwa jina la Sheilla.