Huko kwa Selena, Theroux si poa

UKARIBU uliobuka kati ya Justin Theroux na Selena Gomez, umeibua mjadala mkubwa kuwa huenda wawili hao wameanza kufanya yao.

Hata hivyo, wawili hawa ambao kwa sasa kila mmoja yupo singo baada ya kutengana na mwenza wake, inadaiwa wapo katika harakati za kuanzisha penzi jipya.

Justin, ambaye ndoa yake na Jennifer Anniston ilivunjika miaka miwili iliyopita, ndiye anadaiwa kuvutiwa zaidi na Selena na kuanzisha urafiki ambao, unatafsiriwa kuwa ni uhusiano wa kimapenzi.

Chanzo cha habari kimeeleza kuwa wawili hawa wanaonekana kufurahi uhusiano huo kwa kuwa wote wana vidonda vya kuachana na wapenzi wao.