Muhogo Mchungu aanza kugawa urithi

MWIGIZAJI mkongwe katika tasnia ya filamu Bongo, Abdallah Mkumbila ‘Muhogo Mchungu’ amesema kwa sasa anachofanya ni kuwafundisha sanaa watu wengine kwani siku zote mwanadamu hapaswi kuwa mchoyo kwa kile alichojaaliwa na Mwenyezi Mungu.

“Ni kweli vijana wanajitahidi katika kuigiza lakini bado miiko ya sanaa yenyewe hawana hivyo nimesema wacha nianze kufundisha sanaa kwa kile nilichojaliwa na Muumba,” alisema Muhogo.

Muhogo mchungu alisema kwa kushirikiana na Wakufunzi kutoka chuo kikuu cha Dodoma Grevas Kasiga ‘Chuma’ wameandaa kozi fupi ya wiki mbili kwa vijana wa Mkoa wa Mwanza na inafanyika Shinyanga Hotel.