Kiemba mjanja, atoa mchongo wa maana

Muktasari:

Licha ya nyota wengi wa Ligi Kuu Bara kuwa na majina makubwa wamekuwa hawapati fursa za matangazo tofauti na nyota wa filamu na muziki nchini.

NYOTA wa zamani wa Simba, Amri Kiemba amewapa mchongo wa maana nyota wa Ligi Kuu, juu ya namna ya kutumia vema mitandao ya kijamii ambayo itazishawishi kampuni kadhaa kuwapa matangazo.

Licha ya nyota wengi wa Ligi Kuu Bara kuwa na majina makubwa wamekuwa hawapati fursa za matangazo tofauti na nyota wa filamu na muziki nchini.

“Licha ya kwamba tumechelewa kuamka na kuzitumia vema hizo fursa zilizopo kwenye soka, si vibaya kuamka sasa na kujua thamani ya jina, hii itatokana na jinsi ambavyo watatumia vema mitandao ya kijamii na pia wanavyoishi katika jamii,” alisema.

Alistaajabu kuona watu wasio na majina makubwa ndio wanaopata dili za matangazo, tofauti na wao ambao wanajulikana kila sehemu. “Soka lina heshima,tofauti na wachezaji wanavyolichukulia, upande wangu mitandao ya kijamii ni kwa ajili ya kujifunza na kunufaika kwa kuweka kazi zangu na kujua njia za waliofanikiwa,”alisema.