Msikieni Yesu wa Manchester City

Tuesday August 7 2018

 

MANCHESTER City ya Pep Guardiola imeanza kampeni ya kutetea taji lake la ubingwa wa Ligi Kuu England kwa kuichapa Chelsea 2-0 na kubeba Ngao ya Jamii juzi Jumapili.

Mabao mawili ya Kun Aguero yalitosha kabisa kuizamisha Chelsea kwenye dimba la Wembely jijini London, hivyo kuwa na mwazo mzuri.

Lakini straika wake, Gabriel Jesus ameonya kuwa ushindi huo hauna maana ya kubeba Ngao ya Jamii tu, bali wamejipanga kutetea ubingwa na kipigo kwa Chelsea ni salamu.

Jesus amesema Manchester City itatetea taji hilo mbele ya wababe wengine kwani, ina kikosi bora kama ilivyokuwa msimu uliopita ilipobeba ubingwa kwa tofauti kubwa ya pointi dhidi ya vigogo wengine wa Top Six.

“Utakuwa msimu mgumu kwa timu zote, lakini Manchester City ndio mabingwa watetezi hivyo, bado tuna nafasi nzuri ya kutetea ubingwa wetu.

“Kila timu itakuja kucheza nasi ikifahamu kuwa tunacheza na mabingwa na hiyo itatupa mzuka zaidi wa kutafuta ushindi,” alisema Jesus.

Advertisement