Man U yachomoa mbio za kumnasa Dybala

Monday August 5 2019

 

Manchester ,England. Kwa mujibu wa sky sports imeripotiwa Klabu Manchester united huenda ikaachana na mbio za kutaka kumsajili straika wa timu ya taifa ya Argentina na klabu ya Juventus Paulo Dybala.

Sky sport inaelewa kwamba Manchester united inataka kujiondoa kwene mbio za kumsajilia straika huyo wa Juventus Paulo Dybala kutokana na mahitaji yake ya mshahara na maombi mengi kutoka kwa wakala wa mchezaji huyo.

Aidha Manchester united ilifikia makubaliano na klabu ya Juventus kubadilishana wachezaji wake Paulo Dybala wa Juventus kwenda Manchester united na Romelu Lukaku wa Manchester united kwenda Juventus kwa mujibu wa Sky Italia. Mpango huo ulikuwa unahusu upendeleo wa Dybala na makubaliano yake ya maslahi binafsi  na timu hiyo,hivyo Manchester united kutoridhishwa na maslahi binafsi ya mchezaji huyo.

Lakini kutoridhika kwa United kumsaini Dybala kunaashiria kukomesha ubadilishanaji wowote uliopendekezwa na Juventus kumshirikisha Lukaku. Sky Sports Newsunderstands Manchester United itaendelea kuongea na vilabu vingine juu ya uuzaji wa kimataifa wa Ubelgiji.

Advertisement