Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Musiala amuondolea lawama Donnarumma

MUSIALA Pict

Muktasari:

  • Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 alipata majeraha hayo mabaya baada ya kugongana na kipa wa PSG, Gianluigi Donnarumma, mwishoni mwa kipindi cha kwanza cha mchezo huo uliomalizika kwa PSG kushinda mabao 2-0.

BAYERN, UJERUMANI: STAA wa Bayern Munich, Jamal Musiala amesema “hakuna wa kulaumiwa” baada ya kuvunjika mguu na kifundo cha mguu katika mechi ya robo fainali ya Kombe la Dunia la klabu dhidi ya  Paris Saint-Germain wiki iliyopita.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 alipata majeraha hayo mabaya baada ya kugongana na kipa wa PSG, Gianluigi Donnarumma, mwishoni mwa kipindi cha kwanza cha mchezo huo uliomalizika kwa PSG kushinda mabao 2-0.

Video ya tukio hilo ilionyesha kifundo cha mguu wa nyota huyo wa Bayern kikiwa kati ya mwili na mikono ya kipa huyo wa Italia alipokuwa akikimbilia mpira na inaelezwa kasi ya wachezaji wote wawili ilisababisha jeraha hilo baya linalodaiwa kuwa litamweka nje kwa zaidi ya miezi minne.

Ajali hiyo  ilimwacha Donnarumma akibubujikwa na machozi, akapiga magoti na kuweka mikono yake kichwani akijutia kilichotokea.

Baadaye Donnarumma alichapisha ujumbe kupitia Instagram akimtakia Musiala kila la heri, akiandika: “Maombi yangu yote yapo pamoja na wewe Jamal Musiala10.”

Hata hivyo, kipa wa Bayern Munich Manuel Neuer hakuridhishwa na jinsi Donnarumma alivyoingia kwenye kuuchukua mpira huo na kusema hakujali afya ya Musiala wakati anacheza.

Lakini Musiala, ambaye alisafirishwa kutoka Atlanta, Marekani kurudi Munich kwa ajili ya upasuaji, sasa amesema kuwa hakuna anayepaswa kulaumiwa kwa tukio hilo la kutisha.

“Ningependa kusema asante kwa upendo na msaada wote. Ni jambo la kufurahisha kuona jinsi dunia ya soka inavyokuja pamoja katika nyakati kama hizi. Nimeuthamini sana,” alisema kupitia video aliyoichapisha kwenye Instagram.

“Upasuaji umeenda vizuri sana, niko mikononi mwa wataalamu, na ningependa kusema hakuna mtu wa kulaumiwa kwa hili. Nafikiri hali kama hizi hutokea na sasa nitautumia muda huu kujijenga upya kwa nguvu na mtazamo chanya tena.”

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani anatarajiwa kuwa nje ya uwanja ‘kwa miezi kadhaa ijayo,”  kwa mujibu wa taarifa ya Bayern Munich.

Kocha wa Bayern, Vincent Kompany, alielezea tukio hilo kama ‘la kihisia’  baada ya mechi na kukiri: “Natumai atapata nafuu kwa haraka.”

Musiala alifunga mabao 21 na kutoa asisti 8 katika mashindano yote msimu uliopita ambapo Bayern walipotwaa ubingwa wa Bundesliga.