Huyu Banega anatua Emirates

Sunday June 24 2018

 

WAKALA wa kiungo, Ever Banega, ameripotiwa kutua London kwa ajili ya mazungumzo na Arsenal ili mteja wake akakipige Emirates msimu ujao.

Ripoti zinafichua kwamba staa huyo wa Sevilla amewekwa kwenye orodha ya kocha Unai Emery akimtaka akajiunge na timu yake katika dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi.

Na sasa wakala wake, Marcelo Simonian, amekutana na mabosi wa Arsenal kuzungumzia jambo hilo. Kocha Emery anataka kuongeza nguvu kubwa kwenye sehemu ya kiungo katika kikosi chake cha Arsenal, hivyo anaamini huduma ya Banega mwenye umri wa miaka 29 itafaa zaidi. Arsenal imeshasajili wachezaji wawili; beki wa kulia Stephan Lichsteiner na kipa Bernd Leno.

Jack Wilshere ametangaza kuondoka na Banega anakuja kuziba pengo lake kama watafanikiwa kumsajili.

Advertisement