Mabao kafunga CR7, hela wanabeba Madrid

Friday March 15 2019

 

TURIN, ITALIA,

SI unakumbuka Cristiano Ronaldo amepiga hat-trick dhidi ya Atletico Madrid ile Jumanne iliyopita, basi bana hizo bao tatu alizopiga kwenye mechi hiyo zimewaingizia Real Madrid mkwanja wa Pauni 540,000.

Staa huyo Mreno alifunga mara tatu kuisaidia Juventus kupindua matokeo ya kuchapwa 2-0 na Atletico Madrid katika mechi ya kwanza na hivyo kushinda 3-0 katika mechi ya marudiano na kutinga hatua ya robo fainali.

Iko hivi, kila timu inayoshiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya inapata zawadi ya pesa, ikiwagawanywa kwa timu zote, lakini pesa nyingi zaidi zikienda kwa zile timu zinazoshiriki michuano hiyo na kufika mbali. Timu za Hispania zilipata asilimia 15 ya mgawo wa pesa kwa timu zake kulingana na msimamo wa ligi ulivyo kwa mwaka uliopita. Kwa sababu Atletico ilimaliza juu ya Real Madrid msimu uliopita, basi wao pesa zao zitakuwa nyingi kuliko za Los Blancos kwenye michuano ya Ulaya msimu huu.

Real Madrid imeshatupwa nje na Ajax, lakini bado inapata mkwanja wake.

Real Madrid ianvuna kiasi hicho kwa sababu wakati timu zinafuzu kucheza michuano hiyo msimu uliopita kwenye ligi, staa huyo wa Kireno alikuwa kwenye kikosi cha Real Madrid.

Advertisement