Beckham anyoa kiduku kwa lazima Man United

Friday May 17 2019

 

LONDON, ENGLAND

DAVID Beckham amefichua alivyolazimishwa na Kocha Sir Alex Ferguson kunyoa kiduku chake vyooni Wembley katika mchezo wa Ngao ya Jamii mwaka 2000.

Beckham alisema alitaka kucheza mechi hiyo dhidi ya Chelsea akiwa amenyoa na alimficha Kocha Ferguson kwa wiki nzima kabla ya kuja kushtukiwa muda mfupi kabla ya mechi huko Wembley na kutakiwa kwenda kunyoa haraka.

Beckham alisema: “Tangu nilikuwa na umri wa miaka saba au nane, siku zote nilikuwa nataka kunyoa staili ya nywele ambayo wengine hawakuwa wakinyoa. Nilikuwa nikitaka kuvaa nguo tofauti na wachezaji wenzangu. Nilinyoa kiduku na nilikuwa naogopa kumwonyesha kocha.

“Nilikuwa naenda mazoezini na kofia. Nafanya mazoezi nikiwa na kofia, naenda hotelini na kofia, tunakula chakula cha usiku na kofia, kifungua kinywa asubuhi bado nina kofia, hata kwenye basi tulilopanda kwenda uwanjani, nilikuwa na kofia. Nikaanza kujiandaa na mechi, hapo nikavua kofia. Kocha akaona na kusema: ‘Nenda kanyoe haraka.’ Nikajichekesha na kama kugomagoma hivi, lakini akasema: ‘Niko siriazi, nenda kanyoe.’

“Hivyo, nikatafuta kiwembe, nilienda kunyoa kwenye vyoo vya Uwanja wa Wembley.

Advertisement

Advertisement