Zidane amtaka N’Golo Kante 2020, Pogba pembeni kwanza

Saturday November 30 2019

Zidane- amtaka -N’Golo -Kante -2020-Pogba- pembeni- kwanza-Chelsea-kiungo-real madrid-

 

KOCHA wa Real Madrid, Zinedine Zidane amepania kumnasa kiungo wa Chelsea, Ng’olo Kante dirisha kubwa la majira ya joto mwakani na Madrid wanajiandaa kutoa Pauni 85 milioni kwa ajili ya staa huyo.

Kwa muda mrefu Zidane amekuwa akivutiwa na kiwango cha staa huyo ambaye ni raia mwenzake wa Ufaransa na inadaiwa anamhitaji zaidi pengine kuliko Mfaransa mwingine, Paul Pogba wa Manchester United.

Msimu huu Kante ameendeleza moto na mpaka sasa amefunga mabao matatu katika mechi sita za Ligi Kuu za Chelsea na ingawa mwenyewe amedai hana mpango wa kuondoka lakini hakuna mchezaji asiyetaka kuchezea Real Madrid.

Akitua Madrid, Kante anaenda kuungana na nyota wa zamani wa Chelsea Eden Hazard ambaye Zidane alikuwa akimsaka kwa muda mrefu kabla ya kumnasa dirisha lililopita huku mwenyewe akionekana kuitamani Madrid.

Advertisement