Zahera kulipa kisasi kwa Desabre wa Pyramids

Muktasari:

Mchezo wa mchujo wa kombe la Shirikisho Afrika kati ya Yanga dhidi ya Pyramids FC, utawakutanisha kwa mara nyingine Mwinyi Zahera na Sébastien Desabre.

Dar es Salaam. Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera anakibarua cha kulipa kisasi mbele ya Sébastien Desabre wa Pyramids FC katika mchezo wa mchujo wa Kombe la Shirikisho Afrika, Oktoba 27.

Hii itakuwa mara ya pili kwa Zahera kukutana na Desabre, wawili hao walikutana kwa mara ya kwanza kwenye fainali za mataifa ya Afrika 'AFCON' nchini Misri, Juni 22 katika mchezo wa hatua ya makundi.

Katika mchezo huo wa Kundi A, Zahera akiwa msaidizi wa Florent Ibenge timu ya Taifa ya DR Congo walipoteza kwa mabao 2-0 mbele ya Desabre, aliyekuwa akiinoa timu ya taifa ya Uganda.

Zahera atasimama kama kocha mkuu tofauti na awamu ya kwanza ambapo alikuwa msaidizi huku kwa Desebre akiwa na nguvu kubwa nyuma yake ya usaidizi wa Ramón Diaz, ambaye ni mchezaji wa zamani wa Napoli, Fiorentina, Inter Milan na Monaco.

Nguvu ya fedha ya wapinzani wa Yanga, ilikuwa rahisi