Zahera aitolea uvivu ratiba ya ligi, FA

Thursday March 14 2019

 

Kocha mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera ameitaka Bodi ya Ligi na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuwa na ratiba inayotoa haki kwa Klabu zote. Zahera amesema ameshangazwa kuona mechi za timu yake zipo karibu wakati wao hawana viporo.

Zahera amesema ratiba iliyopo sasa inainyima utulivu wa kufanya mazoezi vyema kutokana na ukaribu wa mechi zao.

Amesema wakati mechi zao zikiwa karibu ameshangaa kuona klabu zingine ambazo zina mechi nyingi za viporo zikipewa muda mrefu wa kupumzika walicheza mechi moja kila baada ya siku sita huku wao walicheza mechi kila baada ya siku tatu.

Aidha Zahera amesema wamejaribu kuongea na Kaimu katibu mkuu wao Omary Kaya kuomba kupewa muda mzuri wa mechi moja mpaka nyingine lakini bodi ya ligi imegoma

 

Advertisement