Yanga Buruguni waichangia Yanga Sh1milioni

Wednesday April 24 2019

 

By Charity James

Dar es Salaam. Wanachama wa klabu ya Yanga, tawi la Buguruni wameichangia klabu yao Sh 1Milion katika kampeni ya changia Yanga iliyoandaliwa maalumu kwaajili ya kuichangia timu hiyo iweze kupata fedha kwaajili ya kusajili msimu ujao.

Kampeni ya changia Yanga iliyochini ya Mwenyekiti Anthony Mavunde ilizinduliwa Dodoma lengo la kampeni hiyo ni kuhakikisha wanakusanya billion 1.5 ambazo ni kwaajili ya kuboresha kikosi chao msimu ujao.

Katibu Mkuu wa tawi la Yanga, Buguruni Shule, Yusuph Yassin alisema Aprili 28 mwaka huu wanachama wote wa tawi hilo wanatarajia kukutana na kuwasilisha kiasi hicho cha fedha ambacho walikiahidi katika uzinduzi wa kampeni hiyo.

"Kulikuwa na utarajibu wa kutolewa kadi kwa kila tawi na sisi tukiwa kama wanachama wa tawi la Buguruni tulichukua kadi ya kiasi hicho ambacho tunaamini hiyo tarehe 28 kitakuwa kimekamilika na tutakiwakilisha siku ya ukamilishaji wa zoezi mwanzoni mwa mwezi wa tano," alisema.

"Kwa ujumla wetu na kwa makubaliano yetu tumeitana kwa lengo moja kuhusiana na michango tuliahidi na tunaimani tutakamilisha kwa wakati lengo ni kuona Yanga yetu inatoka katika upepo mbaya wanaoupitia na kuiingiza katika ushindani hilo linawezekana," alisema Yassin.

Advertisement