Yanga, Azam FC ni kimbembe FA

Friday January 11 2019

 

By THOBIAS SEBASTIAN

YANGA na Azam zijipange, kwani kwenye droo ya raundi ya nne ya Kombe la FA (ASFC) iliyofanyika jana Alhamisi kama zitazubaa kidogo tu, itakula kwao na kuifuata Simba iliyong’olewa mapema tu tena kwa aibu.

Simba iling’olewa na Mashujaa FC ya Kigoma ambayo safari hii imepangwa kupapatuana na Mbeya City mjini Kigoma.

Droo hiyo iliyoshirikisha timu 32, ili kusaka timu za kuingia 16 Bora kabla ya kuisaka Robo Fainali ya michuano hiyo inayotoa uwakilishi wa nchi katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika 2019-2020.

Katika droo hiyo, Yanga imepangwa kuvaana na Biashara United ambayo katika mechi yao ya Ligi Kuu Bara ilihenyeka kupata ushindi kwa wageni hao.

Azam yenyewe imepewa Pamba ya Mwanza ambayo kwa sasa katika Ligi Daraja la Kwanza (FDL) ipo freshi, kitu kinachoonyesha mechi hiyo itakuwa bab’kubwa.

Mechi za raundi hiyo ya nne zitapigwa kati ya Januari 25-28 na baadhi ya viongozi walioshiriki droo hiyo walitoa maoni yao juu ya mechi hizo na namna ambavyo watajipanga kabla ya kukutana na wapinzani wao uwanjani.

Meneja wa KMC FC, Walter Harrison ambayo imepangwa kuvaana na mabingwa wa zamani nchini, Pan Africans, alisema wanafahamu wanakwenda kucheza na timu ngumu iliyoitoa Mwadui kwenye raundi iliyopita, hivyo watawakabili Pan kwa tahadhari kubwa sana.

“Tumepata muda wa kuwafatilia wapinzani na tumewaona kuwa ni timu ngumu na yenye uwezo wa kutoa ushindani, lakini tuna imani tutapata ushindi dhidi yao na kucheza mechi ya hatua inayofata,” alisema Harrison.

Naye Ofisa Habari wa Yanga, Dismas Ten alisema mara baada ya kufahamu wanacheza na Biashara United katika mzunguko wa nne watafanya maandalizi mapema ya mechi hiyo, wakiwa na kumbukumbu ya mechi yao ya Ligi Kuu Bara walivyosumbuka kuifunga.

“Bila ya shaka kocha atafanya majukumu yake, lakini kama viongozi tunakwenda kujipanga ili kuona tunapata matokeo, tunajua Biashara watakuja ili kulipa kisasi cha kufungwa katika ligi,” alisema.

Watetezi wa michuano hiyo Mtibwa Sugar wamepangwa kuanzia nyumbani dhidi ya Majimaji-Songea na kocha wake, Zubeir Katwila alisema; “Malengo ni kama msimu uliopita tu, kubeba ubingwa kwa maana hiyo tumejipanga ili kupata ushindi na kuingia mzunguko wa tano, lakini haitakuwa kazi nyepesi.”

Kocha wa Lipuli Selemani Matola na Meneja wa Azam, Philip Alando waliweka bayana hakuna wanachokifikiria ila kuona wanavuka kwa kushinda.

Ofisa Mashindano wa TFF, Baraka Kiziguto mbali ya kusimamia upangaji wa ratiba na droo ya mzunguko wa nne, lakini ile ya raundi ya ambazo mechi zao zitapigwa mwishoni mwa mezi Februari.

TFF imetangaza fainali ya mwaka huu itafanyika Uwanja wa Ilulu, mjini Lindi mwishoni mwa Mei.

“Tunawasiliana na viongozi wa Lindi na wametuhakikishia uwanja utakuwa tayari kwa matumizi ya fainali na tumeamua kupeleka fainali huko kutokana kutoa fursa kwa mikoa ambayo haina mechi za Ligi Kuu Bara,” alisema Mkurugenzi wa Ufundi za zamani wa TFF, Salum

Advertisement