Winga Al Ahly apenya nyota 23 wa Angola

Wednesday June 12 2019

 

Cairo, Misri. Winga wa Al Ahly, Geraldo ameitwa katika kikosi cha mwisho cha wachezaji 23 wa Angola tayari ya fainali za Mataifa ya Afrika.

Winga huyo mwenye miaka 27, alijiunga na Al Ahly mwezi Januari akitokea katika klabu ya Angola ya CD 1º de Agosto, amekuwa ni mchezaji tegemeo wa miamba hiyo ya Misri.

Geraldo amecheza mechi 17, za Ligi Kuu akihusika katika mabao tisa akifunga matatu na kutegeneza sita.

Geraldo amekuwa ni mchezaji pekee wa kigeni anayecheza Al Ahly aliyefanikiwa kuingia kucheza AFCON baada ya Ali Maaloul na Junior Ajayi kutemwa na timu zao za taifa.

Nyota wa Lazio, Bastos Quissanga, mshambuliaji wa Sporting Braga, Wilson Eduardo, na nahodha Djalma Campos, pamoja na beki wa Sporting Lisbon, Bruno Gaspar wote wameitwa katika kikosi cha mwisho.

Kuachwa kwa beki wa Girona, Jonas Ramalho ambaye amecheza mechi 22 za La Liga msimu huu kumeacha maswali mengi.

Advertisement

Angola imepangwa Kundi E pamoja na Tunisia, Mali, na Mauritania. Mechi yake ya kwanza itacheza dhidi ya Tunisia hapo Juni 24, kabla ya kuivaa Mauritania na kumaliza na Mali.

Kikosi:

Makipa: Toni Cabaça (1º de Agosto), Landu (Interclube), Ndulu (Desportivo da Huíla).

Mabeki: Isaac, Dani Massunguna, Paizo (1º de Agosto), Edy Afonso (Petro de Luanda), Wilson (Petro de Luanda), Bastos (Lazio), Jonathan Buatu (Rio Ave), Bruno Gaspar (Sporting de Portugal).

Viungo: Herenilson (Petro de Luanda), Show, Macaia (1º de Agosto), Stélvio Cruz (F91 Dudelange), Djalma Campos, Freddy (Antalyaspor), Geraldo (Al Ahly).

Washambuliaji: Mabululo (1º de Agosto), Mateus Galiano (Boavista), Wilson Eduardo (Sporting de Braga), Gelson Dala (Rio Ave/Sporting de Porutgal), Evandro Brandão (Leixões).

Advertisement